Keki aliyoandaliwa Serena Williams baada ya kushinda mechi ya 700. |
MIAMI, Marekani
ANDY Murray atacheza na Tomas Berdych katika nusu fainali ya Miami
Open baada ya kumchapa Muaustralia Dominic Thiem.
Mchezaji huyo Mscotland mwenye umri wa miaka 27 alipoteza seti ya
kwanza alipokuwa akicheza na Thiem anayeshikilia nafasi ya 36 duniani, lakini
alitoka nyuma na kuibuka naushindi wa 3-6 6-4 6-1.
Kwa ushindi huo sasa atakutana na mchezaji wa Jamhuri ya Czech
Berdych kwa mara ya kwanza tangu aliposhinda nusu fainali ya mashindano ya Australia
Open Januari.
Naye Serena Williams alipata ushindi wake wa 700 wakati akikata
tiketi ya kucheza nusu fainali baada ya kumchapa Mjerumani Sabine Lisicki.
Murray anayeshikilia nafasi ya tatu kwa ubora, aliyetinga robo
fainali huku akifikisha ushindi wa mechi ya 500 katika historia ya mchezo huo
alipomshinda mchezaji wa Afrika Kusini Kevin Anderson,baada ya kuanza taratibu,
atakutana na Thiem mwenye umri wa miaka 21.
Williams anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora duniani, alimshinda
Lisicki kwa 7-6 (7-4) 1-6 6-3 na kutinga nusu fainali ya mashindano hayo.
Mmarekani huyo amekuwa mchezaji wanane kushinda mchezo wa 700 wa
WTA, ingawa bado you nyuma ya Martina Navratilova mwenye mechi 1,442.
Wachezaji hao wote walikula keki kwa kushinda mechi zao, huku Murray akishindamechi ya 500 wakati mwenzake aliibuka na ushindi katika mechi ya 700.
No comments:
Post a Comment