ISTANBUL, Uturuki
BASI la timu ya Fenerbahce usiku wa kuamkia
leo Jumapili lilipigwa risasi baada ya vinara hao wa Ligi Kuu ya Uturuki
kuibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Rizespor.
Dereva wa basi hilo alijeruhiwa na
kukimbizwa hospitalini lakini hakuna mchezaji aliyeumia katika shambulizi hilo,
ambalo lilitokea wakati timu hiyo ikisafiri kwenda uwanja wa ndege wa Trabzon.
Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu alisema kuwa
uchunguzi utafanyika ili kubaini watu waliohusika na tukio hilo.
Nayo Shirikisho la Soka la Uturuki
lililaani shambulizo hilo na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Mahmut Uslu alisema
tukio hilo halikuwa sahihi.
"Tulikuja hapa kucheza mchezo,
tulikuja hapa kucheza soka, " alisema Uslu.
Abdulcelil Oz, ambaye ni gavana wa Trabzon huko
kaskazini-mashariki ya Uturuki, awali alisema basi hilo lilionekana kama
lilipigwa na jiwe lakini baadae alitoa taarifa nyingine, akisema kuwa,
inaonekana lilipigwa risasi.
"Hali ya sasa inaonekana ilikuwa
bunduki," alisema Oz. "Ni mapema mmno kusema lolote kwa sasa, lakini
ni aina ya risasi kutoka katika bunduki aina ya."
Kundi kubwa la mashabiki wa Fenerbahce walikuwa
wakiisubiri timu hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Istanbul kuwapokea wachezaji
wao wakirejea kutoka katika mechi hiyo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye
ni mnazi mkubwa wa Fenerbahce, aliripotiwa akimtaka gavawa wa eneo hilo kufanya
uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Fenerbahce ndio mabingwa watetezi wa ligi
hiyo na wameshinda taji hilo mara 19, huku baadhi ya wachezaji wake wazamani
kama akina Dirk Kuyt, Raul Meireles na Emre katika kikosi hicho.
Huko Istambuli yaliko maskani ya klabu hiyo
ambayo imepanga kileleni katika msimamo wa ligi hiyo baada ya ushindi huo wa
Jumamosi, pointi moja mbele ya wapinzani wao wakubwa Galatasaray.
No comments:
Post a Comment