*Wanarudiana na Maafande wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa
Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, Yanga (pichani), leo wanashuka katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam
kucheza na maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Yanga wanashuka uwanjani
huku wakiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare na maafande hao katika mchezo wa
raundi ya kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja huohuo.
Vijana hao wa kocha Hans
van der Pluim wameshinda mechi sita mfululizo huku leo kikosi cha Mkenya Tom Olaba
kitakuwa na kibarua cha kuwalinda vikali washambuliaji wenye uchu wa mabao wa
Yanga.
Baadhi ya
washambuliaji wake hao ni Simon Msuva, Amissi
Tambwe, Kpah Sherman
na Mrisho Ngassa, ambao wamekuwa wakifunga mabao kama hawana akili nzuri na kuiwezesha
Yanga kucheza mechi zao za mwisho mwisho kwa kishindo.
Timu hiyo yenye
pointi 49 kileleni, inahitaji pointi sita tu ili kuivua ubigwa Azam FC, huku
ikisubiri kucheza Polisi Morogoro Jumatatu, Azam FC itacheza nao Mei 6 kabla ya
kuhitimisha kwa kucheza na Ndanda FC ugenini Mei 9.
Yanga wanatofautiana
na Ruvu Shooting kwa pointi 20 ikiwa na maana kuwa vijana hao wa Jangwani hadi
sasa wamejikusanyia jumla ya pointi 49 wakati wapinzani wao hao wa leo wana
pointi 29 tu.
Hakuna ubishi kuwa maafande
hao wamekuwa hawana matokeo mazuri katika baadhi ya mechi zao zilizopita, baada
ya kufungwa na Kagera Sugar 2-0 kabla ya kuja kuifunga Mgambo Shooting 2-1
katika mchezo uliopita.
Timu zote mbili
zitakumbuka kuwa zilichezeana rafu mchezo wa kwanza, kiasi cha kusababisha
baadhi ya wachezaji kupigwa faini kwa utovu wa nidhamu.
No comments:
Post a Comment