LIBREVILLE, Gabon
MIAKA, miezi, wiki hatimaye siku zimepita kabla ya kesho Jumamosi kuanza
kwa fainali za 31 za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini hapa na
kushirikisha jumla ya nchi 16 zinazowania taji hilo.
Leo katika ufunguzi wa mashindano hayo kutakuwa na mechi mbili, lakini
moja ile itakayoanza saa moja usiku na kuzikutanisha Burkina Faso na Cameroon
ndio itakayovuta hisia za wapenzi wengi wa soka.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 4:00 Usiku na kuutangulia ule
utakaowakutanisha wenyeji Gabon dhidi ya Guinea-Bissau utakaofanyika kuanzia
majira ya saa 1:00 Usiku, ambapo mechi hizo zote za Kundi A, zitapigwa kwenye
Uwanja wa Uwanja wa Stade d'Angondjé.
Beki Bakary Kone, kiingo na
nahodha Charles Kabore na mshambuliaji Jonathan Pitroipa kati yao wamecheza
mechi 173 na watakuwa wakitegemewa zaidi.
Hatahivyo, Cameroon inashiriki mashindano hayoya Afcon huku ikiwakosa
wachezaji wake nane, akiwemo beki wa Liverpool Joel Matip, aliyegomea kuichezea
timu ya taifa lake.
Benjamin Moukandjo ndiyer aliyefanywa nahodha mpya kwa Simba hao
wasiofungika.
Preview ya
Mchezo
Nchi hizo katika historia ya soka la Afrika zimekutana mara moja tu
wakati bao la Alphonse Tchami lilipoipatia Cameroon ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
wenyeji Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi wa fainali za mwaka 1998.
Cameroon imeshinda mara nne taji la mashindano hayo, katika miaka ya 1984,
1988, 2000 na 2002, wakati Burkina Faso ilikaribia kabisa kulitwaa taji hilo
mwaka 2013 wakati walipomaliza katika nafasi ya pili.
Nchi hizo zote mbili zitatakwa kugangamala na kuimarika zaidi baada ya kushiriki
fainali za mwisho mwaka 2015 walipotolewa katika hatua ya makundi. Cameroon
walitoka sare mara mbili na kupyeza mchezo mmoja, wakati Burkina Faso ilitoka
sare mara moja na kupoteza mara mbili.
Kocha Hugo Broos amemfanya mfungaji wa wakati wote wa Cameroon Lorient
scorer Moukandjo kama nahodha wake mpya.
MAKOCHA WANASEMAJE
Kocha wa Cameroon Hugo Broos: "Wakati wote ni muhimu kaunza kwa
ushindi. Unaposhinda mchezo wa kwanza unakuwana nafasi ya asilimi 50 ya kuwa na
uhakika wa kucheza raundi ya pili.
"Lakini itakuwa ngumu sana kusonga mbele, kwani Burkina Faso miaka
michache iliyopita ilicheza fainali za Mataifa ya Afrika na hatutakiwi kuwadharau, kwani ni timu nzuri.”
RATIBA KESHO JUMAMOSI:
Gabon v Guinea-Bissau Stade d'Angondje 1:00 Usiku
Burkina Faso v Cameroon Stade d'Angondje 4:00 Usiku
Jumapili, Januari 15, 2017
Algeria v Zimbabwe Stade de Franceville 1:00 Usiku
Tunisia v Senegal Stade de Franceville 4:00 Usiku
Jumatatu, Januari 16, 017
Cote d'Ivoire v Togo Stade d'Oyem Saa 1:00 Usiku
DR Congo v Morocco Stade de Franceville Saa 4:00 Usiku
Jumanne, Januari 17, 2017
Ghana v Uganda Stade de Port Gentil Saa 1:00 Usiku
Mali v Misri Stade de Port Gentil Saa 4:Usiku
No comments:
Post a Comment