ALIYEKUWA Kocha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ Charles Mkwasa amesema kilio chake kimesikika na hatimaye Tanzania imepangwa kwenye kundi rahisi kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2019.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkwasa ambaye ameifundisha Taifa Stars
akirithi mikoba ya kocha Mdenmark Mart Nooij amesema timu ambazo zipo kundi
moja na Tanzania ni rahisi ukilinganisha na kundi la msimu uliopita ambapo
ilipanga na Nigeria na Misri.
“Timu zilizopangwa kundi moja na Tanzania ni timu za kawaida
ukilinganisha na Misri au Nigeria lakini maandalizi ya mapema ni muhimu ili
kufanya vizuri,” alisema Mkwasa.
Pia Mkwasa alisema pamoja na kuonekana kuwa rahisi lakini kitendo cha
nchi hizi kuwa na viwango vinavyokaribiana kinaweza kufanya iwe ngumu zaidi kwa
maana ya kukamiana.
“jukumu linabaki kwa shirikisho la Soka (TFF), wachezaji pamoja na benchi
la kiufundi kujiandaa kwani nilisema hadharani tumekuwa tukipangwa kwenye kundi
la kifo ila droo ya sasa CAF walisikia kilio changu na inawezekana iwapo
tutaamua,” alisema Mkwasa.
Tanzania imepangwa Kundi L pamoja na vinara wa soka ukanda wa Afrika
Mashariki Uganda, Lesotho na Cape Verde, ambapo wengi wanasema ni jepesi
ukilinganisha na huko nyuma ilibyokuwa ikipangwa Stars.
Kwa upande wa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' ambayo ipo ukanda
huu wa Afrika Mashariki imepangwa kundi F sambamba na Ghana, Ethiopia na Sierra
Leone.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema ratiba
hiyo ni faraja kubwa kwa Tanzani kwani wadau wa soka wakiungana na TFF, “hakuna
shaka tunaweza kufuzu kwa fainali hizo za 2019.”
Hatahivyo,Lucas alisema pamoja na kuwepo katika kundi linaloonekana
jepesi, lakini bado maandalizi ya Stars yanatakiwa kuwa makubwa kwani Uganda na
Cape Verd bado ni timu nzuri.
Alisema kuwa Uganda Cranes ni timu nzuri na itakuwa na hamu kubwa ya
kucheza tena fainali hizo za mwaka 2019 baada ya kushiriki zile za mwaka huu
nchini Gabon, ambazo zinaanza leo.
Wenyeji wa michuano hiyo Cameroon ambayo imefuzu moja kwa moja imepangwa
kundi B pamoja na Morocco, Malawi na mshindi kati ya Comoro na Mauritius.
Wakati huo huo; timu za Sao Tomé, Madagascar, Comoro, Mauritius, Djibouti
na Sudan Kusini wataanzia kwenye mechi za mtoano Machi na mataifa matatu
yataingia kwenye hatua za makundi.
Jinsi makundi yalivyopangwa:
Kundi A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar
Kundi B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoro/Mauritius
Kundi C: Mali, Gabon, Burundi, Djibouti/Sudan Kusini.
Kundi D: Algeria, Togo, Benin Gambia.
Kundi E: Nigeria, Afrika Kusini, Libya, Shelisheli.
Kundi F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya.
Kundi G: DR Congo, Congo Brazzaville, Zimbabwe, Liberia.
Kundi H: Ivory Coast, Guinea, Jamhuri ya Afrika ya kati, Rwanda
Kundi L: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania.
No comments:
Post a Comment