Ni kifo Morocco, Ivory
Coast
KOCHA wa timu ya taifaya Morocco
Herve Renard amebainisha kuwa watapambana kufa au kupona wakati watakapokutana
na timu yake yazamani ya Ivory Coast kesho katika mchezo wa Afcon.
Miaka miwili baada ya
kuiongoza Ivory Coast kutwaa taji hilo, Renard itakabiliana nao katika robo
fainali ya michuano hiyo.
"Najaribu kusahau, kwasababu
nilipowaiona Waivory coast kabla ya kufuzu kwa Kombe la Dunia miezi miwili
iliyopita, ilikuwa ni hisia kali kwangu, “alisema.
"Ilitubidi kupambana na
kucheza ili kushinda…tulitakiwa kuwa na nguvu.”
Renard ambaye ni kocha wa Morocco
iliifunga Togo 3-1 katika mchezo wa Kundi c Ijumaa na kujiweka katika mazingira
mazuri, ikifuatiwa na sare ya Ivory Coast na Congo (DR) ya bao 2-2 katika
mchezo wa mapema siku hiyo.
Congo (DR) ndio wanaoongoza
kundi hilo wakiwa na pointi nne, Ivory Coast mbili wakati Togo ikiwa na pointi
moja.
Ushindi dhidi ya Ivory Coast katika
mchezo utakaofanyika Oyem utaiwezesha Morocco kufuzu kwa hatua ya nane bora,
lakini hadi sasa timu zote nne katika kundi hilo zina nafasi ya kufuzu.
Morocco ilijiweka katika
hatari mjini Gabon, baada ya kufungwa mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya
Congo na kuwa nyuma ya Togo Ijumaa kabla ya kubadili matokeo na kushinda 3-1.
Renard aliwapongeza wachezaji
wake baada ya kupambana hadi kupata matokeo ambayo yameiweka pazuri timu hiyo.
No comments:
Post a Comment