Broos siku moja kurejea
Cameroon
KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon
Hugo Broos anataka Joel Matip kurejea katika timu ya taifa baada ya kumalizika
kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika.
Matip alikataa wito wa
kuichezea Cameroon katika mashindano hayo ya Afcon na badala yake akaenda
kuichezea Liverpool.
"Nafikiri atabadili
mawazo yake na tutamuona katika mchezo ujao (baada ya kumalizika kwa Afcon) kwa
sababu ni mchezaji mzuri sana, “alisema Broos.
Sheria za Fifa zinasema kuwa
mchezaji huenda akazuiwa kuichezea klabu yake endapo atakataa kuichezea nchi
yake lakini Ijumaa Matip alishafisha kuichezea klabu yake.
Broos aliongeza: "Nina furaha
sana kuwa hili tatizo limetatuliwa na anaweza kuichezea tena Liverpool na nina
tumaini anaweza kuichezea tena Cameroon.
"Nafikiri kila mmoja yuko
huru kufaya uamuzi na kuamua kutokuja nasi hapa katika mashindano ya Mataifa ya
Afrika.
"Kwa kweli naheshimu
uamuzi lakini pia nafikiri Shirikisho la Soka la Cameroon kimefanya kile
kilichofanya kwa kufuata sheria za Fifa na ni rahisi sana kusema hapa…
"Lakini tatizo hilo sasa
limetatuliwa, kwangu hakuna tatizo zaidi nab ado nina tumaini kama nilivyofanya
tangu nilipokuwa kocha wa Cameroon, atakuja na kucheza nasi tena.”
Matip hajaichezea Cameroon tangu
mwaka 2015 na hajakuwemo katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya
mashindano hayo.
Cameroon inaongoza katika
Kundi A na ilikuwa ikihitaji pointi moja kutoka katika mchezo wao wa mwisho
dhidi ya wenyeji Gabon jana ili kufuzu kwa robo fainali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment