Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na kamati ya Olympic Tanzania TOC, wamezindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Tokyo, nchini Japan mnamo mwaka 2020.
Uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa karume jijini Dar
es salaam umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Michezo Nchini, Yusuph Omari ambaye
alikua mgeni rasmi, Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Jamal
Malinzi, Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Henry Tandau,
maafisa wa TFF na wadau wengine wa michezo.
kampeni hiyo inayoihusisha timu ya taifa ya soka ya vijana
chini ya umri wa miaka 20 (Kilimanjaro Worriers) ambayo itawania kufuzu kucheza
michuano ya Olimpiki mwaka 2020, imepewa jina la ‘The Road to Tokyo 2020’.
Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema dhamira kubwa
waliyojiweka katika harakati hizo ni kuhakikisha vijana wanaendelezwa kisoka
kwa ajili ya kufikia malengo ya kwenda kushiriki michuano ya Olimpiki mwaka 2020.
Mkurugenzi wa
michezo Yusuph Omari “Nimesikia
program mbalimbali za TFF, naona zinakuja wakati mwafaka. Niwapongeze kwa
mipango yenu mizuri kwa sababu inaleta matumaini. Jambo kubwa ambalo linanisukuma
na kuwapongeza ni kuwa na program ya vijana, hatuwezi kufanikiwa kama
hatutakuwa na program ya vijana.
No comments:
Post a Comment