Kocha Mali awajibika kwa
kipigo
KOCHA wa Mali Alain Giresse amesema
kuwa kwa timu yake 1-0 na Ghana katika mchezo wa Kundi D katika mashindano ya
Afcon yanayoendelea ni kosa lake.
Mfaransa huyo alisema kuwa
angeweza kufanya vizuri zaidi katika uteuzi wa timu dhidi ya Black Stars ambao
sasa wamefuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
“Nawajibika kwa kipigo hicho dhidi ya Ghana.
Ningeweza kufanya vizuri zaidi kwa kutumia wachezaji wa akiba hivyo hakuna
ubishi hilo ni kosa langu, “alisema Giresse ambaye kikosi chake kina pointi moja tu baada
ya mechi mbili na kikosi katika nafasi ya tatu.
Chipukizi Yves Bissouma,
Moussa Doumbia na Kalifa Coulibaly, walioanzia katika benchi, waliingizwa
katika kipindi cha pili na kuonesha kiwango kizuri.
Mbinu binafsi za Bissouma na Doumbia
ziliishangaza Ghana baada ya majaribio kadhaa ya kipa Razak Brimah,na kama
wangeanzia kipindi cha kwanza wangeweza kupata bao.
“Sio tatizo
la kujiamini ila ni uzoefu tu. Ilikuwa rahisi kwao kuja na jua kuwa wanaweza
kucheza vizuri kwa sababu ilikuwa hatari. Ni vizuri kama wangeingizwa mapema na
bila shaka wangefanya vizuri, “alisema
Giresse.
Mali itakabiliana na Uganda
katika mchezo mwisho wa Kundi D utakaofanyika Stade d’Oyem keshokutwa, ambapo timu zote bado hazijafunga
wala kushinda katika Afcon 2017.
No comments:
Post a Comment