KAMPALA, Uganda
KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Milutin 'Micho' Sredojevic (pichani), amelitaka
Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) kutimiza
masharti ya mkataba la sivyo atawachukulia hatua za kisheria.
Mserbia huyo, ambaye aliipeleka Uganda Gabon katika mashindano ya Kombela
Mataifa ya Afrika (Afcon 2017), kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kufuzu
kwa takribani miaka 39, amesema anadai malimbikizo ya mishahara yake.
Micho alisema kuwa wanaweza kulimaliza suala hilo vizuri, lakini kama
wakishindwa basi atakimbilia katika vyombo vya kisheria.
Chini ya Micho the Cranes ilitolewa katika hatua ya makundi ya Afcon 2017
nchini Gabon baada ya kufungwa kiduchu na vigogo wa Afrika Ghana na Misri kabla
ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mali.
Kiwango cha timu hiyo ya Uganda kilikuwa kizuri sana na kinaonesha dalili
kuwa, timu hiyo imeimarika zaidi, hasa ukilinganisha na timu hiyo iliposhiriki
mashindano hayo kwa mara ya mwisho mwaka 1978.
Kocha huyo amekuwa akihusishwa na nchi kibao zikiwemo Ghana – baada ya
kocha wa the Back Stars, Avram Grant akijiandaa kuondoka baada ya mashindano
hayo ya Mataifa ya Afrika.
"Nina mkataba hadi wakati wa mashindano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019
lakini wakati wote mabeki ya makocha huwa nusu yameshapangwa vitu tayari kubaki
na tayari kuondoka,”alisema Micho.
"Uganda inatakiwa kuamua. Kwa kweli niko wazi kwa kila kitu kwa
sababu zimekuja ofa nyingi.
No comments:
Post a Comment