MSHINDI wa mbio za Mumbai Marathon, Alphonce Simbi
amesema kuwa ili Tanzania ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali ya
kimataifa, lazima wajiandae vizuri na kushirikisha wanariadha wengi.
Sambu aliyasema hay oleo wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika hafla maalum ya kumpongeza iliyoandaliwa na Kampuni
ya Multichoice jijini Dar es Salaam, ambayo pia ilihudhuria na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi.
Alisema kuwa kujiandaa vizuri na idadi kubwa ya
wanariadha wanaotoka nchi moja katika shindano husika kunasaidia kufanya vizuri
kama wanavyofanya Kenya.
Simbu aliwashukuru sana DStv kwa kumdhanini kwani
kumesaidia kufanikisha kutimiza ndoto yake ya kufanya vizuri katika mashindano
makubwa ya kimataifa.
Alisema Wakenya wamekuwa wakipeleka wanariadha wengi
katika mashindano na kwa mfano katika mbio hizo za Mumbai Marathon ilikuwa na
zaidi ya wakimbiaji saba, ambao walisaidia sana katika mbio.
Alisema kuwa alimuacha Mkenya katika kilometa 41,
ambapo chomoka na kumaliza wa kwanza katika mbio hizo, ukiwa ni ushindi wake wa
kwanza katika mbio za marathon.
Simbu aliwashukuru DStv, Riadha Tanzania, mwajiri
wake ambaye ni Jeshi la Kujenga Taifa, Waandishi wa Habari na wadau wengine
wote wa michezo kwa ushirikiana wao uliomuwezesha kufanya vizuri.
Pia aliomba watu wengine wajitokeze kuwasaidia
wanariadha kwa njia mbalimbi ikiwemo kuwapatia maji au mafuta ya magari au
pikipiki na vitu vingine ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano
tofauti tofauti.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice, Shelukindo
alimpongeza Simbu kwa ushindi huo wa Mumbai Marathon, ambapo alisisitiza kuwa
wataendelea kumsaidia mwanariadha huyo.
Alisema kuwa waliamua kumsaidia Simbu baada ya
kushika nafasi ya tano katika Michezo ya Olimpiki ya Rio 2016 ili aweze kufanya
vizuri zaidi katika mashindano mengine makubwa licha ya baadhi ya watu
kutotuelewa kwanini tunamsaidia mtu aliyeshika nafasi ya tano.
Alisema kuwa Multichoice itaendelea kumsaidia Simbu,
ambapo watajitahidi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanachangia
sekta zote za michezo na burudani.
Aliwataka waadishi wa habari kuendelea kuandika mema
ya nchi yetu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye alisema kuwa baada ya Simbu kufanya vizuri alihisi kuwa sasa ututukufu
wa Tanzania katka riadha umerudi.
Pia aliwapongeza DStv kwa kuwa wazalendo wa kweli
katika kuhakikisha michezo inasonga mbele hapa nchini.
Alisema mafanikio ya Simbu ni mfano hai kuwa watu
wakiwekeza vizuri mafanikio yataonekana, ambapo aliwapongeza Multchoice kwa
msaada wao kwa Simbu.
Alitoa wito kwa wadau wengine wa michezo kujitokeza
kuwasaidia wachezaji mbalimbali hapa nchini ili waweze kufanya vizuri.
Alisema watu wa utalii wakiwekeza kutumia wizaya ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kujitangaza badala ya kutumia fedha nyingi
kwa matangazo.
No comments:
Post a Comment