LONDON, England
JOSE Mourinho amewakosoa wachezaji wake kwa kushangilia kupita kiasi bao
la kwanza la Juan Mata wakati Manchester United ikiibuka na ushindi katika
mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Hull City.
Manchester United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiweka katika
nafasi nzuri ya kutinga fainali ya mashindano hayo.
Iliwachukua Man United dakika 56 kuvunja ngome ya Hull City na kufunga
bao katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Mata alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira wa kichwa uliopigwana
Henrikh Mkhitaryan.
Bao hilo liliwafanya wachezaji wa Man United kushangilia kwa muda mrefu,
kitendo ambacho kilimkera Mourinho ambaye alibainisha hilo baada ya mchezo huo.
"Tulitakiwa kucheza badala ya kutumia muda mrefu kushangilia bao,
“alisema kocha hiyo alipozungumza na Sky Sports. "Katika kila mchezo wa
kombe kila bao ni muhimu hivyo kwanini mnashangilia wakati mna nusu saa ya
kucheza?
"Sifiki kama tulitakiwa kufanya vile, hakuna sabbau ya kushagilia
bao la kwanza namna ile.”
Maelezo hayo yalikuja wakati Mourinho akiwataka wachezaji na mashabiki wa
timu yake kuelekeza nguvu zao katika mchezo ujao dhidi ya Liverpool katika
mchezo wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Old
Trafford utakaofanyika Jumapili.
Alipoulizwa kama alikatishwa tama na kiwango cha timu yake katika kipindi
cha kwanza, kocha huyo wa United aliongeza: "Ndio kidogo. Kwa kweli
hatukuwa katika kiwango chetu kipindi cha kwanza.
"Ndio, Hull walijipanga vizuri kama nilivyotarajia na haikuwa rahisi
kwetu….”
No comments:
Post a Comment