Ghana yasonga mbele wakati Uganda ikiaga mashindano Gabon 2017
WAKATI Ghana ikitinga robo
fainali ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayoendelea Gabon,
wawakilishi wa Afrika Mashariki Uganda wametolewa.
Asamoah Gyan aliiongoza Ghana
katika hatua inayofuata ya mtoano baada ya kuifungia bao lililoiwezesha timu
hiyo kuibuka na ushindi dhidi ya Mali kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa
mapema juzi.
Gyan alifunga bao hilo pekee
katika mchezo huo wa Kundi D kwa kichwa katika mchezo uliofanyika hapa.
Katika mchezo mwingine,
mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo, Misri wenyewe walimtumia mchezaji
aliyetokea benchi Abdallah El Said na kufunga katika dakika ya 89 na kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda.
Kwa kipigo hicho, Uganda ndio
imekuwa timu ya kwanza kabisa kukata tiketi ya kurudi nyumbani.
Ghana ambao ni mabingwa mara
nne, ambao walimaliza katika nafasi ya pili mwaka 2015, ni timu pekee ya pili
ya kufuzu kwa robo fainali, wakati nyingine ni Senegal.
"Katika mashindano
unahitajika kushinda mechi na hilo ndilo tulilofanya leo, “alisema Gyan, ambaye sasa amefunga katika fainali sita
za Mataifa ya Afrika.
"Tumeridhishwa na kiwango
chetu. Ama tumecheza mchezo mzuri au la, muhimu ni kushinda na kusonga mbele."
Baada ya ushindi mfululizo wa
baoa 1-0, kikosi cha kocha Avram Grant kitamaliza cha kwanza endapo kitakwepa
kufungwa wakati watakapocheza na Misri katika mchezo wa mwisho wa kundi lao
utakaofanyika keshikutwa Jumatano.
Timu zilizuiwa kufanya mazoezi
kabla ya kuanza kwa mechi ili kuepuka kuharibuka zaidi eneo la kuchezea, ambapo
mchezo ulipoanza Ghana ndio walizoea haraka hali ya mchezo.
Andre Ayew nusura afunge bao
baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Christian Atsu lakini alipiga juu, kabla
bao pekee halijafungwa katika dakika ya 21.
Gyan alifunga kwa akichwa
akiunganisha krosi ya Jordan Ayew likiwa ni bao lake la nane katika mashindano
ya Mataifa ya Afrika, ambapo bao lake la kwanza alilifunga mwaka 2008 wakati
fainali hizo zilipofanyikia Ghana.
Mali, ambao walitolewa katika
hatua ya makundi baada ya kutoka sare nyingi mwaka 2015, sasa wanatakiwa
kuifunga Uganda katika mchezo wa mwisho na huku wakiombea kufungwa kwa Misri
kama wanataka kuendelea kuwepo katika mashindano.
Misri wenyewe wanahitaji
pointi moja tu ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua inayofuata baada ya
ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Uganda Jumamosi usiku.
Kikosi cha kocha Hector Cuper
kilitoka suluhu na Mali katika mchezo wao wa kwanza na baadae kuonekana kama
ingetoka tena sare ya bila kufungana hadi pale Mohamed Salah alipomtengenezea
mchezaji aliiyetokea benchi El Said aliyefunga bao hilo.
Ni pigo kwa Uganda ambao
walifungwa kwa penalty katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ghana na kujikuta
wakimaliza mchezo wakiwa nyuma kwa bao 1-0 baada ya juzi kushindwa kuondoka na
pointi hata moja.
No comments:
Post a Comment