Mechi za hatua ya Makundi zimemalizika na tayari tumepata timu
zinazoendelea mbele kwenye hatua ya Robo Fainali:
Robo fainali zinaanza leo Januari 28, 2017:
Timu zilizofanikiwa kuendelea mbele kwenye hatua ya Robo fainali ni
pamoja na; Burkinafaso, Tunisia, Senagal,
Cameroon, Misri, DR Congo na Ghana.
Jumamosi hii, 28/01/2017 tutashuhudia Robo Fainali za kwanza kati ya :
• Burkinafaso dhidi ya
Tunisia saa 12 jioni SS Select 2 (DStv 234)
• Senegal dhidi ya Cameroon
saa 3.30 Usiku SS Select 2 (DStv 234)
Wakati Robo Fainali za pili zitafanyika Jumapili ya tarehe 29/01/2017
kati ya
• DR Congo dhidi ya Ghana
saa 12 jioni SS Select 2 (DStv 234)
• Misri dhidi ya Morocco
saa 3.30 usiku SS Select 2 (DStv 234)
Matokeo ya Kushangaza
Hakuna aliyetarajia kuwa mabingwa watetetezi (Ivory Coast) wangeondolewa
haraka kwenye mashindano haya mapema mno pamoja na kuwa na kikosi chenye
wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaofanya vizuri katika ligi mbali mbali
duniani.
Sababu kubwa ukiachilia
mfumo wa uchezaji ni kukosekana kwa Ari ya Ushindi na ushindani ndani ya timu.
Kikosi cha Ivory Coast kilikosa kiongozi uwanjani na pengine ni kutokana na
kustaafu kwa wachezaji wao nguli kama ndugu wawili watokao kwenye familia ya
Toure; Yaya na Kolo; Hawa walitegemewa kuleta chachu zaidi kwenye timu na
kuleta uongozi ndani ya timu.
Wachezaji kama Eric Bailly, Wilfried Zaha, Serge
Aurier, Wilfried Bony, Max Gradel na Salomon Kalou wote hawa walishindwa
kuipatia ushindi timu yao na taifa lao kwa ujumla. Ivory coast imeaga
mashindano haya bila kushinda mechi hata moja.
Kutolewa mapema mno kwa
Algeria ni matokeo mengine yaliyoshangaza wengi. Riyad Mahrez alishindwa kabisa
kusaidia timu yake na hivyo kushindwa kuthibitisha ubora wake kama mchezaji
bora wa Africa kwa mwaka huu.
Wachezaji wenzake kwama Islam Silmani, Nabil
Bentaleb na Yacin Brahimi wote walishindwa kuibeba timu yao. Ngome yao ya
ulinzi ilionekana kupwaya na kukosa mawasiliano hasa katika idara ya kiungo cha
ukabaji. Algeria walionekana wakicheza kibinafsi Zaidi na kutegemea juhudi
binafsi kuliko timu.
Utabiri Wangu wa Robo Fainali
• BurkinaFaso Vs Tunisia
Tunisia ana nafasi kubwa zaidi ya Burkinafaso kwa kuangalia aina ya
wachezaji,uchezaji na matokeo ya mechi zilizo tangulia. Mpaka kufikia robo
fainali; Tunusia ameshinda mechi 2 na kupoteza 1 wakati Burkinafaso ameshinda 1
na kutoka sare mbili
• Senegal Vs Cameroon
Senegal ni timu iliyoonyesha mpira mzuri sana katika mashindano haya na
wanacheza kitimu Zaidi na wanaonyesha mipango ya ushindi kila wanaposhika
mpira. Ninawapa nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Cameroon. Mpaka kufikia Robo
fainali; Senegal wameshinda mechi 2 na kutoka sare 1 wakati Cameroon wametoka
sare 2 na kushinda 1. Hata hivyo hii ni moja kati ya Robo fainali zuri na ngumu
sana; chochote kinaweza kutokea
• Misri Vs Morocco
Moja kati ya Robo fainali ngumu sana; majirani wawili kutoka Africa
kaskazini wanakutana, waarabu wawili wanaocheza mpira wa kuvutia na wenye kasi
na wanaotumia akili sana. Matokeo yoyote yanaweza tokea, ingawa naona ushindi
kuamuliwa kwa mikwaju ya penati. Natoa nafasi kubwa kwa Misri; mpaka kufikia
hatua hii Misri ameshinda mechi 2 na kutoka Sare 1 wakati Morocco ameshinda
mechi 2 na kupoteza 1
• DRC Congo Vs Ghana
Majirani zetu Congo wameonyesha kiwango kizuri sana cha soka huku
wakicheza kwa umoja na maelewano makubwa. Uwezo wao wa kumiliki mpira na uwanja
hasa kwenye eneo la kati umewafanya wawe
timu bora kabisa.
Ghana nao si haba, wameonekana kucheza kwa umoja ingawa bado kuna hali ya
utegemezi kwa baadhi ya wachezaji; hata hivyo ni timu nzuri na yenye kuvutia.
Nashawishika kusema hii itakuwa Robo fainali bora pengine kuliko nyingine zote
ukizingatia viwango vya uchezaji, mbinu, ufundi na ubora ulioonyeshwa na timu
zote mbili
Ninawapa nafasi kubwa sana jirani zetu DRC Congo kufanya vizuri kwenye
mchezo huu dhidi yay a Ghana. Mpaka kufikia hatua hii, Congo wameshinda mechi 2
na kutoka sare 1 huku Ghana ikishinda mechi 2 na kupoteza 1
Usikose uhondo huu, Ungana nasi (DStv) kupitia chaneli yetu ya Supersport
kushuhudia mechi hizi Live bila chenga ndani ya SS6 na SS Selekti kwa vifurushi
vyote
Unangoja nini sasa? Uhondo huu unazidi kunogeshwa na Robo fainali, wahi
sasa jipatie king’amuzi chako bora kabisa cha DStv na ushuhudie uhondo huu moja
kwa moja kutoka Gaboni bila chenga wala mikwaruzo yeyote ile ndani ya DStv HD
kwa shilingi 79,000 tu na malipo ya shilingi 19,975 tu kwa mwezi; DStv Bomba.
No comments:
Post a Comment