ABUJA, Nigeria
MSHAMBULIAJI wa Leicester Riyad Mahrez ndiye mchezaji bora wa Afrika kwa
mwaka 2016, Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limetangaza.
Mchezaji huyo wa Algeria mwenye umri wa miaka,25, aliyeisaidia Leicester
kutwaa taji la Ligi Kuu ya England, tayari ndiye mchezaji bora wa PFA wa mwaka
na yule wa BBC.
Mshambuliaji wa Gabon anayeichezea klabu ya Borussia Dortmund,
Pierre-Emerick Aubameyang alikuwa wa pili na Msenegal wa Liverpool Sadio Mane
alimaliza watatu katika mbio hizo za kuwania uchezaji bora.
Mshambuliaji wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi alishinda tuzo ya mchezaji
chipukizi wa mwaka.
Mchezaji mwingine wa Nigeria anayekipiga katika klabu ya Manchester City,
Kelechi Iheanacho alikuwemo katika orodha ya wachezaji waliokuwa wakiwania
heshima hiyo.
Mahrez, 25, alimshinda nahodha wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye
alipata heshima hizo mwaka jana, lakini juzi aliishia katika nafasi ya pili.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ufaransa alisema kuwa ni heshima kubwa sana
kwake kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka uliomalizika.
"Ni heshima kuubwa, nina furaha na ninashukuru. Nawashukuru
wachezaji wenzangu wote Leicester na Algeria," alisema Mahrez wakati
akipokea tuzo hiyo.
"Natoa tuzo hii kwa familia yangu na wote wanaoniunga mkono kila
siku.”
Leicester ilishangaza pale ilipotwaa ubingwa wa England wakati ilikuwa
haipewi nafasi yoyote hata ya kubaki katika ligi hiyo msimu uliopita.
Mahrez alifanya kazi kubwa katika klabu yake baada ya kufunga mabao 17 na
ksaidia kupatikana kwa 10 katika mechi 37 alizoichezea timu hiyo.
Alikuwa mchezaji wa kwanza wa Algeria kushinda taji la Ligi Kuu na kupata
mapokezi makubwa aliporejea nyumbani Algeria, ambako kwa mara ya kwanza
alifikiriwa kuwa ni mchezaji wa rugby alipotakiwa kujiungta na timu hiyo miaka
minne iliyopita.
Wachezaji wote watatu waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa
mwaka wa Afrika pia walichaguliwa katika kikosdi cha CAF cha wachezaji 11,
ambacho pia kinaundwa na beki wa Ivory Coast Eric Bailly wa Manchester United.
Kipa Denis Onyango alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ndani baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Mamelodi
Sundowns Khama Billiat na Mzambia Rainford Kalaba.
Onyango alifanya vizuri wakati klabu yake ya Mamelodi Sundowns ilipotwaa
taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika, na kuisaidia timu ya taifa ya Uganda `The
Cranes’ kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), baada ya kutokuwepo
kwa muda mrefu.
Mnigeria Asisat Oshoala alitwaa tuzo yake ya pili ya mchezaji bora wa
mwaka wa Afrika kwa wanawake baada ya kuisaidia Nigeria kutetea taji la Afrika
nchini Cameroon.
Nyota huyo wa timu ya wanawake ya Arsenal alishinda kwa mara ya kwanza
tuzo hiyo wakati pia alipoweza kuisaidia Super Falcons kutwaa taji la Afrika
mwaka 2014.
Wachezaji chipukizi wa Nigeria Kelechi Iheanacho na Alex Iwobi walitwaa
tuzo ya wachezaji wanaochipukia vizuri na ile ya wachezaji chipukizi wa mwaka.
Mwamuzi wa Gambia Bakary Papa Gassama alishinda tuzo ya mwamuzi bora kwa
mara ya tatu mfululizo.
WASHINDI WA
TUZO
Mchezaji bora
wa Afrika wa mwaka
Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
Mchezaji bora
wa mwaka anayecheza Afrika
Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
Mchezaji bora
wakike wa mwaka
Asisat Oshoala (Nigeria & Arsenal)
Chipukizi
mwenye kipaji cha aina yake
Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City)
Chipukizi bora
wa mwaka
Alex Iwobi (Nigeria & Arsenal)
Kocha bora wa
mwaka
Pitso Mosimane (Mamelodi Sundowns)
Klabu bora ya
mwaka
Mamelodi Sundowns
Timu bora ya
taifa ya mwaka
Uganda
Timu bora ya
taifa ya wanawake
Nigeria
Mwamuzi bora wa
mwaka:
Bakary Papa Gassama
Kikosi cha CAF
cha wachezaji 11 wa 2016
Kipa: Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
Mabeki: Serge Aurier (Cote d’Ivoire & PSG), Aymen
Abdenour (Tunisia & Valencia), Eric Bailly (Ivory Coast & Manchester
United) na Joyce Lomalisa (DRC &AS Vita).
Viungo: Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns),
Rainford Kalaba (Zambia & TP Mazembe), Keegan Dolly (Afrika Kusini &
Mamelodi Sundowns).
Washambuliaji: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia
Dortmund), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Riyad Mahrez (Algeria &
Leicester City).
Wachezaji wa
akiba: Aymen Mathlouthi (Tunisia
& Etoile du Sahel), Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli), Salif
Coulibaly (Mali & TP Mazembe), Islam Slimani (Algeria & Leicester
City), Mohamed Salah (Misri & Roma), Kelechi Iheanacho (Nigeria &
Manchester City) na Alex Iwobi (Nigeria & Arsenal)
No comments:
Post a Comment