MANCHESTER, England
MSHAMBULIAJI wa Manchester United Anthony Martial anatakiwa
"kunisikiliza mimi na sio wakala wake ", anasema kocha wa timu hiyo Jose
Mourinho.
Wakala huyo Mfaransa aliripotiwa hivi karibuni
akisema kuwa “anaangalia” uwezekano wa mteja wake kuhamia katika klabu ya
Sevilla ya Hispania.
Martial,mwenye umri wa miaka 21, alikuwa mfungaji
bora wa Man United msimu uliopita baada ya kufunga mabao 17, lakini bao lake la
kusawazisha alilofunga jana Jumamosi wakati Manchester United ikiibuka na
ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Middlesbrough
lilikuwa ni bao lake la tano kufunga msimu huu.
"Ni mchezaji wa ajabu na wa aina yake alikuwa
mfungaji bora msimu uliopita, “alisema Mourinho.
"Martial alicheza, alitengeneza, pia alifunga.
Alipambana, ni mchezaji mzuri. Najua ana kipaji cha hali ya juu sana.”
Martial, aliyejiunga na Man United akitokea Monaco kwa
ada ya pauni mioni 36 mwaka 2015, alifanya kazi nzuri wakati timu yake ikitoka
nyuma Jumamosi na kuibuka na ushindi huo dhidi ya Boro.
Alisawazisha kwa bao la dakika 85 kabla ya Paul Pogba
hajafunga lile la ushindi dakika moja baadae.
Baadae, Mourinho alishauri kuwa Martial anatakiwa
kufuata mfano wa mchezaji mwenzake wa timu hiyo Henrikh Mkhitaryan, aliyetakiwa
na kocha wake kufanya zaidi, ambapo alijibu kwa kufunga mabao matatu katika
mechi nne zilizopita.
Kocha huyo wazamani wa Chelsea aliongeza kusema:
"Nilijua Mkhitaryan ni kipaji cha hali ya juu lakini nilikuwa simchezeshi.
Kwa kipindi hiki hucheza hata beki ya kushoto wakati timu ikishinda na
tunahitaji kulinda ushindi wetu na kuhitaji balansi zaidi.
"Martial anatakiwa kunisikiliza mimi na sio
wakala wake. Anatakiwa anisikilize mimi katika mazoezi kila siku na katika kila
mrejesho ninaompa kujaribu kumuimarisha na kumboresha zaidi.
"Huku Martial kika kukiha nasoma magazeti, 'Anthony Martial anakwenda Sevilla, Anthony
Martial anakwenda kucheza kwa mkopo, Anthony Martial hana furaha'. Anthony
Martial anachotakiwa ni kunisikiliza mimi na sio mtu mwingine yeyote.”
Beki wazamani wa United Phil Neville: "Nafikiri
ni kitu rahisi. Klabu imewekeza kwa mchezaji huyo kiasi cha pauni milioni 56.
Sasa ni jukumu lake kumuuliza wakala wake kwa nini anamuhusisha na kuhamia Sevilla
na aseme kwa sasa niko katika moja ya klabu kubwa kabisa duniani. Nataka
kuendelea kubaki Man United.”
Nahodha wazamani wa timu ya taifa ya England Alan
Shearer: "Martial alikuwa mchezaji bora katika mchezo ule na aliweza
kuirejesha Man United mchezoni. Na alicheza vizuri tangu mwanzo wa mchezo.”
No comments:
Post a Comment