LONDON, England
KOCHA Mkuu wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameshtakiwa na Chama cha
Soka (FA) kwa madai ya kutoa lugha chafu na kumsukuma mwamuzi wa akiba wakati
wa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Burnley.
Wenger alimsukuma mwamuzi msaidizi, Anthony Taylor baada ya kutolewa nje
katika mchezo huo,a mbao uliofanyika Jumapili na Arsenal kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1.
Kocha huyo alijikuta akitolewa nje baada ya kufoka katika dakika ya 93
kufuatia penalti waliyopewa Burnley, ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo, Burnley walifikiri kuwa kwa mara ya pili wangeweza
kuondoka na pointi moja ugenini msimu huu baada ya Andre Gray kufunga bao la
kusawzisha kwa penalti baada ya Francis Coquelin akiadhibiwa kwa kumchezea
vibaya Ashley Barnes.
Hatahivyo, the Gunners ndio walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya
Shkodran Mustafi kufunga bao la kuongoza katika kipindi cha pili akiunganisha
wavuni mpira wa kona iliyochongwa na Mesut Ozil akifunga bao lake la kwanza
katika soka la Uingereza.
Alexis Sanchez ndiye aliyekuwa mkombozi wa Arsenal katika mchezo huo
baada ya kuudokoa mpira katika dakika ya 98 na kumpita Tom Heaton baada ya Ben
Mee kupigiwa filimbi kufuatia kumrushia daruga Laurent Koscielny, ambaye
alionekana akiwa katika nafasi ya kuotea.
Kwa upande wa Wenger, 67, kocha huyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo
huo aliomba radhi na amepewa hadi Alhamisi awe amejibu tuhuma hizo.
Taarifa ya FA ilisomeka: "Inadaiwa kuwa katika dakika ya 92, Wenger alitumia
lugha chafu au za kukera dhidi ya mwamuzi wa akiba.
"Inadaiwa zaidi kuwa kufuatia kutolewa nje kutoka eneo la ufundi,
kocha huyo aliendeleza ujeuri katika njie ya kuingilia katika vyumba vya
kubadiishia nguo baada ya kumsukuma mwamuzi msaidizi…”
Baada ya kutakiwa na mwamuzi Jon Moss kwenda kukaa jukwaani, Wenger aliondoka
kutoka uwanjani lakini alisimama kati njia ya kuingilia na kugoma kutoka
akijaribu kuangalia sehemu iliyobaki ya mchezo kutoka hapo, ambapo Taylor alijaribu
kumshawishi kuondoka lakini badala yake alimsukuma mwamuzi huyo msaidizi.
No comments:
Post a Comment