LONDON, England
TIMU ya Swansea City imeteremka daraja baada ya
misimu saba kucheza Ligi Kuu ya England, baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1
dhidi ya Stoke City, ambayo tayari ilishatangulia katika Ligi Daraja la Kwamza.
Swansea City imemaliza ligi hiyo inayoshirikisha
jumla ya klabu 20 ikiwa katika nafasi ya 18 baada ya kujikusanyia jumla ya
pointi 33 ikiwa pointi sawa na Stoke City iliyopo katika nafasi ya 19 huku West
Bromwich Albion ikishika mkia ikiwa na pointi 31.
Klabu hiyo ya Welsh ilihitaji mabo 10 ili iweze
kubadili matokeo na kuiporomosha Southampton, kitu ambacho haikutokea na
kushangaza yenyewe ndio imeporomoka baada ya misimu saba ya kucheza ligi hiyo.
Lakini hadi mapumziko, Swansea City, ambayo
haijashinda mchezo wowote ugenini katika mechi 13 zilizopita, iliongoza kwa bao
la Msenegal Badou Ndiaye na baadae Peter Crouch. Xherdan Shaqiri walifunga kwa
Stoke huku pia ikikosa penalti.
Kocha Mreno wa Swansea City, Carlos Carvalhal ana
nafasi kubwa ya kuondoka katika klabu hiyo, miezi mitano tangu aanze
kuifundisha.
"Jana nilizungumza na mmiliki, jana Jumatatu
tulitarajia kuzungumza tena, “alisema.
"Mimi mwenyewe nitafikiria kuhusu Swansea na
nitazungumza na famnilia yangu. Baada ya hapo nitatoa uamuzi sahihi kuhusu hatma
yangu.
"Najua Ligi Daraja la Kwanza na tulifikia hatua
ya mchujo mara mbili. Hiyo sio kawaida timu kucheza mchujo mara mbili
mfululizo.”
Kocha wa Stoke City Paul Lambert naye pia muda wake
wa kuifundisha timu hiyo haukutosha kubadili mambo baada ya kuanza kuifundisha
timu hiyo Januari.
"Kuna mambo hayako vizuri, hilo halina wasiwasi,
“alisema.
No comments:
Post a Comment