LONDON, England
MSHAMBULIAJI
wa Liverpool Mohamed Salah (pichani) ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Soka.
Kiungo wa Manchester
City Kevin de Bruyne ameshika nafasi ya pili huku mshambuliaji wa Tottenham Harry
Kane akiibuka watatu.
Salah, mwenye
umri wa miaka 25, amefunga mabao 31 katika mechi 34 za ligi alizoichezea timu hiyo
msimu huu.
Nyota huyo wa
Misri, ni mwanasoka wa kwanza wa Afrika kupewa tuzo hiyo, ambaye pia alitwaa
tuzo kutoka kwa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa mwezi uliopita.
Mshambuliaji
wa Chelsea na England Fran Kirby ameshinda tuzo ya uchezaji bora wa mwaka kwa
wanawake (FWA).
Salah amefunga
mabao 43 katika mashindano yote baada ya kusajiliwa na Liverpool kwa ada ya
uhamisho ya pauni milioni 34 akitokea Roma ya Italia.
Mchezaji huyo
wazamani wa Chelsea na Basel alifunga mara mbili katika mchezo wa kwanza wakati
Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Roma katika mchezo wa nusu
wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwenye Uwanja wa Anfield wiki iliyopita.
Kikosi cha
kocha Jurgen Klopp tayari kiko Italia kwa mchezo wa Jumatano dhidi ya Roma
utakaofanyika kwenye Uwanja wa Stadio Olimpico kwa ajili ya mchezo huo wa
marudiano.
MBIO ZA WACHEZAJI WAWILI
Salah na
mchezaji mwenye umri wa miaka 26 Mbelgiji De Bruyne alipata zaidi ya asilimia
90 ya kura zilizopigwa na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Soka.
Mwenyekiti wa
FWA Patrick Barclay alielezea mpambano wa wawili hao kama ni wa nguvu zaidi
tangu mwaka 1968-69", wakati walipopambana kati ya Tony Book wa Manchester
City na yule wa Derby, Dave Mackay.
Wachezaji
wengine waliopigiwa kura na wanachama wa FWA walikuwa: Sergio Aguero (Man
City), Christian Eriksen (Tottenham), Roberto Firmino (Liverpool), Nick Pope
(Burnley), David Silva (Manchester City), Raheem Sterling (Man City) na Jan
Vertonghen (Tottenham).
No comments:
Post a Comment