LONDON, England
KOCHA Antonio Conte anadai Chelsea haina nafasi ya
kushinda fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United isipokuwa kama
itajiimarisha haraka baada ya kuhoji uwezo wa wachezaji wake.
Kocha huyo Mhitalia alisema kikosi hicho kinatakiwa
kuboreshwa baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Newcastle United
Jumapili na kumaliza msimu vibaya na kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya.
Kikosi cha Conte kilikuwa na nafasi ya kumaliza ligi
juu ya nafasi ya tano, lakini sasa watacheza Ligi ya Ulaya, wana nafasi ya
kutwaa taji wakati watakapocheza dhidi ya Man United kwenye Uwanja wa Wembley
Mei 19.
Hilo linatarajia kuwa pambano la mwisho kwa Conte
katika kikosi hicho cha Chelsea, ambacho kitacheza dhidi ya kocha wao wazamani Jose
Mourinho, kocha huyo mwenye umri wa miaka 48
anajua kuwa klikosi chake kinahitaji kuinua kiwango chake katika idara
zote ili kutwaa taji kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.
"Tulitaka kumaliza msimu katika njia nzuri,
lakini tungeweza kufanya vizuri zaidi ya hivi, “alisema.
"Kwa hilo, nimekuwa wa kwanza kujibu kuhusu
mchezo mbovu. Newcastle walionesha mchezo mzuri na kupambana, na kama tutacheza
kama hivi katika fainali ya Kombe la FA, basi kamwe hatutakuwa na nafasi.
"Tuna siku sita tu kubadili muelekeo wetu, na
tunatakiwa kupambana kwasababu tunaweza kufanya vizuri zaidi.”
Amebakisha miezi 12 kabla ya kumalizika kwa mkataba
wake wa sasa, na alipoulizwa kuhusu hatma yake, kocha huyo wazamani wa timu ya
taifa ya Italia aliongeza: “Nina mkataba, na najituma na klabu inajua kila
kitu.
"Mchezo wa Jumamosi ndio utakuwa wa mwisho? Hapana,
sifikiri hivyo. Kitu muhimu ni klabu, na sio uvumi kuhusu mimi.”
No comments:
Post a Comment