LONDON, England
MOHAMED Salah ameweka rekodi mpya ya kufunga mabao
katika Ligi Kuu baada ya kupachika mabao 32 katika mechi 38 alizocheza na
kuuhakikishia Liverpool nafasi ya kurejea katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Brighton katika
mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Anfield.
Ushindi huo kwa Liverpool unamaana kuwa haijalishi
Chelsea imepata matokeo gani katika mchezo wake dhidi ya Newcastle United,
lakini ilifungwa mabao 3-0 katika mchezo wake uliofanyika kwenye Uwanja wa St
James's Park.
Chelsea hata kama ingeshinda bado isingeweza kumaliza
katika nafasi ya nne, kwani Liverpool ilitakiwa kufungwa ndio Chelsea ifuzu kwa
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao.
Liverpool imepania kutwaa taji la sita Ulaya wakati
itakapokutana na Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Mei
26.
Lakini vijana wa Jurgen Klopp wanajua kuwa hata kama
hawata twaa taji katika fainali hiyo huko Kiev, watarejea katika Ligi ya
Mabingwa msimu ujao baada ya kuisambaratisha Brighton ugenini katika mchezo wa
mwisho wa Ligi Kuu ya England.
"Sasa tuko katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
msimu ujao na nimepata tuzo pia, hivyo ninajivunia sana, “alisema Salah wakati
akikabidhia tuzo ya kiatu cha dhahabu kwa ufungaji bora katika Ligi Kuu ya
England.
Mabingwa wapya Manchester City imevunja rekodi ya
ushindi, kupata pointi nyingi na mabao mengi msimu huu na kuwa timu ya kwanza
ya Uingereza kufikia rekodi ya pointi 100 wakati Gabriel Jesus alipofunga bao
la dakika za mwisho wakati wakiifunga Southampton 1-0.
Man City pia imeweka rekodi katika Ligi Kuu kwa kuwa
na pointi nyingi dhidi ya timu inayofuatia ya Manchester United, ambayo
ilishinda bao 1-0 dhidi ya Watford kwenye Uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment