Mwandishi
Maalum
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imeanza mikakati ya kujiwekea mfumo wa
viashiria hatarishi (Risk Management) kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake,
ambayo yameanza jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) uliopo Kipawa jijini Dar es Salaam.
Akifungua
mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, ambayo yanashirikisha
washiriki kutoka Idara mbalimbali, Bw. Lawrence Thobias ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa
yatatumika kama sehemu ya kazi, hivyo washiriki wote wazingatie na kujifunza
kwa bidii.
“Ninajua
wote waliopo kazini wanauwezo na nyie mmechaguliwa wachache na hamuwezi kuja
wote katika mafunzo haya, ila ninachowaomba mjifunze kwa bidii na mshirikishane
yale mnayoyafahamu, kwani wote hapa ni wazoefu ili kuleta ufanisi bora na mzuri
katika Taasisi yetu,” amesema Bw. Thobias.
Bw.
Thobias amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, TAA itatengeneza nyaraka
za viashiria hatarishi kwa kutumia wataalamu watakaochaguliwa miongoni mwa
washiriki, ambazo zikikubalika kwa viwango vinavyotakiwa, basi itatakiwa
kusimamiwa na kuendeshwa vyema na Mamlaka.
Naye
Naibu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (Usimamizi wa Viashiria Hatarishi,
Mfumo na Udhibiti wa Ndani), kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu Bw. Emmanuel Subbi
kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu, amesema wameamua kutoa mafunzo ya viashiria
hatarishi (Risk Management) kwa Taasisi za Serikali ili waweze kuishauri Serikali
namna ya kuvizuia na kuvidhibiti kabla ya kutokea.
Bw.
Subbi amesema kila Taasisi inatakiwa kuwa na mwongozo wa viashiria hatarishi wa
mwaka 2013 na pia Waraka wa Hazina namba 12 wa mwaka 2013, ambapo zote
zinaonesha namna na jinsi ya kuzuia viashiria hatarishi.
“Mfumo
huu una faida kubwa kwa Taasisi za Umma kwani unasaidia kuaminika na hata
kupata mikopo kutoka katika Taasisi mbalimbali Duniani, pia mfumo huu utakupa
nafasi nzuri ya kufanya maamuzi kwa upana ikiwa unaangalia na mfumo wako wa
kazi,” amesema Bw. Subbi.
Pia
Bw. Subbi amesema mfumo huu utasaidia kuepuka matatizo katika ununuzi, sheria,
viwango na udhibiti, ambapo miaka ijayo itapunguza kupatikana kwa hati chafu
kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), ambapo mfumo ukizingatiwa hakutakuwa
na matatizo hayo kwani watagundua viashiria hatarishi kabla havijatokea na
kuleta madhara.
No comments:
Post a Comment