LONDON, England
JURGEN Klopp amepata pigo kubwa kuelekea mchezo wao
wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Roma baada
ya msaidizi wake muhimu Zeljko Buvac kuachia ngazi kutokana na sababu za
kibinafsi.
Huku Liverpool ikiwa mbioni kukabiliana na Roma
katika mji mkuu wa Italia Jumatano usiku, klabu hiyo imethibitisha juzi kuwa Buvas
atakuwa nje ya timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
Klopp alimuelezea Buvas kama "kichwa" katika
suala zima la ukocha na kutokuwepo kwake ni pigo kubwa kwa Liverpool ambayo
inaangalia kuendelea ushindi wake wa awali wa mabao 5-2 dhidi ys Roma.
Tetesi zilianza kusambaa tangu Jumapili kuwa Bosnian anaachia
ngazi, lakini Liverpool ilikanusha taarifa hizo kwa kusisitiza kuwa Buvac bado
ni muajiriwa wa klabu hiyo na pengo lake halitaathiri kitu.
Buvac, ambaye alikuwa katika benchi pamoja na Klopp katika
mchezo wa Jumamosi ambao timu hiyo ilitoka suluhu dhidi ya Stoke, alikuwa
msaidizi wa karibu kabisa wa kocha huyo Mjerumani katika kipindi cha miaka 17
iliyopita.
Wawili hao walikuwa pamoja huko Mainz katika miaka ya
1990 na waliungana tena wakati Klopp alipomfanya kuwa msaidizi wake wakati
alipokuwa kocha mwaka 2001.
Wakati alivyopanda pamoja wawili hao walienda Borussia
Dortmund mwaka 2008 ambako walishinda mfululizio taji la Bundesliga na kucheza
fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kabla hawajahamia Liverpool.
Wakati
huohuo, leo inashuka nchini Italia kucheza dhidi ya Roma
katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Kikosi cha Klopp
kiko mbioni kutinga fainali baada ya kuwa na faida ya mabao mengi iliyopata
katika mchezo wa kwanza ilipoifunga Roma mabao 5-2, ikiwa ni mara ya kwanza
tangu mwaka 2007 walipofikia hatua ya juu ya mashindano makubwa Ulaya.
Lakini nje ya
uwanja presha ni kubwa wakati shabiki wa Liverpool Sean Cox lyuko katika koma
baada ya kushambuliwa kabla ya mchezo wa wili iliyopita uliofanyika kwenye
Uwanja wa Anfield.
Mashabiki
wawili wa Roma walikamatwa kuhusiana na jaribio hilo la kutaka kuuwa na gwiji
wa klabu hiyo Francesco Totti ametaka kuwepo kwa mchezo wa kiungwana, na
kuheshimiwa kwa wapinzani.
Mshambuliaji
wazamani wa Roma Mohamed Salah alifunga mara mbili na kutengeneza mengine
mawili wakati Liverpoo; ikizifumania nyavu mara tano kwenye Uwanja wa Anfield kabla
ya mawili yaliyofungwa katika dakika za mwisho.
Kikosi cha Klopp
kitashuka uwanjani bila ya kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye atakuwa nje
ya uwanja kwa msimu mzima kutokana na maumivu ya goti, pamoja na Georginio
Wijnaldum ambaye alibadilishwa katika mchezo wa kwanza.
Emre Can (mgongo)
na Adam Lallana (maumivu ya nyama za paja) nayo pia wanapambana na maumivu.
No comments:
Post a Comment