TIMU ya taifa
ya Misri itacheza dhidi ya Kuwait kesho Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa
kirafiki kati ya 15 itakayochezwa na timu hiyo ya Afrika iliyofuzu kucheza Kombe la Dunia
itakayofanyika kuanzia Juni 14hadi Julai 15 nchini Urusi.
Timu za taifa
ya Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia zinaliwakilisha bara ya Afrika
katika Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi.
MIsri
watamkosa mkali wao Mohamed Salah huko Kuwait City wakati akiichezea klabu yake
ya Liverpool ambayo leo inacheza dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa fainali
ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya leo.
Nyota
mwingine wa Kombe la Dunia, Sadio Mane wa Senegal, naye pia atakuwa katika jezi
ya Liverpool akijaribu kuizuia Real Madrid kutwaa taji lake la nne mfululizo la
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Baada ya
kucheza na Kuwait, kikosi hicho cha timu ya taifa ya Misri ambacho
kinafundishwa na kocha wa Argentina Hector Cuper atakiongoza kwenda Ulaya
kucheza na Colombia huko Milan na baadae Ubelgiji jijini Brussels.
Morocco, imerejea
katika Kombe la Dunia baada ya miaka 20 ya kutokuwepo, itakwaana na timu ambazo
hazijafuzu kwa Kombe la Dunia Ukraine na Slovakia katika jiji la Uswisi la Geneva
kabla ya kukabiliana na Estonia huko Tallinn.
Nigeria ndio
nchi pekee ya Afrika ambayo itacheza mchezo wa kujipima nguvu barani, ikiikaribisha
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Port Harcourt Jumatatu hii.
Timu hiyo ya 'Super
Eagles' baadae itakabiliana na England kwenye Uwanja wa Wembley na Jamhuri ya Czech
huko Austria kabla haijapanda ndege na kwenda Urusi, nchi ya kwanza ya Ulaya
Mashariki kuandaa fainali za Kombe la Dunia.
Senegal, inashiriki
kwa mara ya pili baada ya kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na kutinga robo
fainali, itacheza dhidi ya Luxembourg na Croatia kabla haijakutana na Korea
Kusini bila wachezaji kwenye Uwanja wa Australia.
Tunisia, bila
kushinda mechi 14 za Kombe la Dunia tangu ilipowafunga Mexico mwaka 1978, watakuwa
ugenini wakicheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ureno kabla hawajakutana na
Uturuki huko Uswisi na Hispania huko Urusi.
Nchi tani za
Afrika zilizofuzu zinarejea mchezoni kwa mara ya kwanza tangu Machi wakati
walipopata matokeo tofauti tofauti walipocheza mechi za kirafiki.
Misri
ilichapwa 2-1 na Ureno baada ya Cristiano Ronaldo kufunga mara mbili katika
muda wa majeruhi na timu hiyo iliyobadilika sana ilijikuta ikifungwa 1-0 na
Ugiriki.
Morocco iliwafunga
Serbia 2-1 huko Italia na kurejea nyumbani ambako walishinda 2-0 dhidi ya Uzbekistan.
No comments:
Post a Comment