Nahodha wa England, Harry Kane. |
MOSCOW, Urusi
HADI mashabiki 10,000 wa soka kutoka England
wanatarajia kutua nchini hapa mwezi ujao ili kuiunga mkono timu yao itakapokuwa
ikicheza mechi za Kombe la Dunia mwaka huu, amesema msemaji wa Ubalozo wa Uingereza
mjini hapa juzi.
Msemaji huyo akizungumza na Shirika la Habari
la Urusi, Tass, alisema kuwa wanatarajia raia karibu raia 10,000 kutoka
Uingereza kutembelea Urusi mwaka huu kwa ajili ya kuja kushuhudia fainali za
Kombe la Dunia.
“Tunatarajia karibu wapenzi wa soka 10,000
kutoka Uingereza kutembelea Urusi mwaka huu kuja kushuhudia fainali za Kombe la
Dunia na kuja kufurahia uhusiano mzuri kati ya Uingereza na Urusi kabla ya
Kombe la Dunia kwa miaka miwili sasa.
"Ofisa wa usalama Mark Roberts (ambaye
anashughulikia sera za soka) alitembelea mara mbili nchini Urusi mwaka jana,
“alisema. “Msafara wa Polisi wa Uingereza walifanya kazi wakati wa mechi za
Kombe la Shirikisho la Dunia kwa Klabu
Julai mwaka jana.
Gazeti la Uingereza la Daily Star wiki hii
liliandika ripoti kuwa mashabiki wa soka wa England watakuwa wakitafuta kitu
huko Urusi wakati wa Kombe la Dunia na hilo litakuwa kama Vita ya Tatu ya
Dunia, Nne, Tano, Sita na Saba.”
Vurugu kadhaa
ziliripotiwa kati ya mashabiki wa soka wakati wa mashindano ya Kombe la Uefa
huko Ufaransa kati ya Juni 10 na Julai 10, 2016. Mpambano mkubwa uliowahi
kuibuka kati ya mashabiki wa Urusi na Waingereza wakati ikielekea mechi ya Juni
11 huko Marseilles.
Fainali za Kombe la Dunia 2018 zinatarajia
kuanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi huku mechi ya ufunguzi ikitarajiwa
kupigwa mjini hapa.
Urusi imechagua miji 11 kuchezwa fainali
hizo, ambayo ni Moscow, St. Petersburg, Sochi, Kazan, Saransk, Kaliningrad,
Volgograd, Rostov-on-Don, Nizhny Novgorod, Yekaterinburg na Samara.
No comments:
Post a Comment