HAVANA, Cuba
ZAIDI ya watu
100 wamekufa baada ya ndege aina ya Boeing 737 kuanguka jirani na kiwanja
kikubwa cha ndege cha Cuba mjini hapa, ikiwa ni ajali mbaya zaidi ya anga kuwahi kutokea katika miongo kadhaa.
Wanawake
watatu waliokolewa wakiwa hai kutoka katika mabaki ya ndege hiyo, lakini wakiwa
katika hali mbaya sana.
Ndege hiyo,
ambayo inakaribia umri wa miaka 40 tangu itengenezwe, ilikuwa imepakia abiria
104 na wafanyakazi sita.
Mamlaka ya
Cuba imeanzisha uchunguzi, huku ikitangaza siku mbili za maombolezo kutokana na
ajali hiyo.
Ndege hiyo
aina ya Boeing 737-201 iliyokuwa ikifanya safari za ndani, ilianguka majira ya
saa 10:08 jioni juzi, muda mfupi baada ya kupaa kutoka katika Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha José Martí jijini Havana
wakati ikienda kwenye Kiwanja cha Frank Pais huko Holguin, mashariki ya kisiwa
hiki.
Wafanyakazi
wote wa ndege hiyo walikuwa ni raia wa Mexico, huku abiria wengi wakiwa ni raia
wa Cuba, huku miongoni mwao walikuwa abiria watano wakigeni.
"Kuna
ajali mbaya ya anga imetokea. Habari hazifurahishi na inaelekea kuna idadi
kubwa ya abiria wamekufa, “alisema Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel alipotembelea
eneo la tukio, ndege hiyo ilipoangukia.
Nini sababu za ajali?
Taarifa
zilisema kuwa ni mapema mno kusema sababu za ajali hiyo, lakini mashuhuda waliokuwa
chini walielezea kuwa waliiona ndege hiyo ikilipuka kabla ya kuanguka msituni
jirani na kiwanja kikubwa cha ndege cha Havana.
"Niiona
ndege hiti ikiruka, “alisema mfanyakazi mmoja wa duka kubwa Jose Luis aliliambia
Shirika la Habari la AFP. “Mara, iligeuka, na kuanguka chini. Wote
tulishangaa.”
"Tulisikia
mlipuko na badae tuliona moshi mkubwa ukieenda juu, “alisem aGilberto Menendez,
ambaye anaendesha mgahawa mmoja jirani na eneo lililotokea ajali hiyo.
Idara ya
usafiri ya Mexico ilisema katika mtandao wake kuwa “wakati ikipaa (ndege hiyo)
ilipata matatizo na kurudi chini.”
Kampuni ya Boeing
ilisema kuwa iko tayari kupeleka timu ya mafundi Cuba kwa ajili ya kufanya
uchunguzi wa kina kujua tatizo lililoisibu ndege hiyo hadi kuanguka.
Watu Walionusurika
Waru wanne
walinusurika katika jail hiyo lakini mmoja alikufa mara baada ya kufikishwa
hospitalini, alisema mkurugenzi wa hospitali ya Calixto Garcia iliyopo Havana, Carlos
Alberto Martinez.
Watui hao
watatu walionusurika wote ni wanawake, kwa mujibu wa gazeti la Chama cha
Kikomunisti la Granma: mmoja akiwa na
umri kati ya miaka 18 na 25, wakati mwingine mwenye umri wa miaka 13 wakati
watatu ana miaka 39.
"Yuko
hai lakini ameungua vibaya, “alisema ndugu ya mwanamke huyo katika hospitali
hiyo.
Nchi zote, Argentina
na Mexico zilithibitisha kuwa wananchi wa mataifa yao ni miongoni mwa waliokufa
katika ajali hiyo.
Tunachijua Kuhusu Ndege
Ndege hiyo
ilitolewa na kampuni ya Mexico ya Aerolines Damojh kwa shirika la ndege la
serikali la Cuba la Cuban de Aviación.
Mamlaka ya
Mexico ilisema kuwa ndege hiyo ilitengenezwa mwaka 1979 na ilikaguliwa Novemba
mwaka jana. Mexico imesema kuwa imetupa wataalam wawili wa mabo ya anga
kusaidia katika uchunguzi huo.
Aerolineas
Damojh, ambayo pia inajulikana kama Global Air, ina ndege tatu ambazo zinafanya
kazi.
Ajali Zingine za Ndege
Kwa mujibu wa
tafiti, mwaka jana ndege ya biashara ambayo ilikuwa ikisafiri bila abiria,
ilianguka. Lakini mwaka huu kumekuwa na ajali kibao mbaya za ndege.
Mwezi
uliopita, ndege ya jeshi ilianguka na kuua zaidi ya watu 250. Februari , ndege
ya Saratov Airlines ilianguka karibu na Moscow, iliua watu 71 mwezi Machi,
ndege ya Marekani ya Bangla Airlines ilianguka Kathmandu, Nepal; iliua watu 51.
Ajali
nyingine mbaya ya ndege ilitokea mwaka 1989, wakati ndege ya abiria iliyotengenezwa nchini Urusi aina ya Ilyushin-62M
ilianguka jirani na jiji la Havana na kuua abiria wote 126 waliouwemo ndani ya
ndege hiyo na wengine 24 waliokuwa ardhini.
No comments:
Post a Comment