Na Mwandishi Wetu
PAZIA la Ligi
Kuu Tanzania Bara litafungwa usiku wa Jumatatu ya Mei 28, mwaka huu
kwa mchezo kati ya Yanga SC na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Taarifa ya
Mkurugenzi wa Bodi wa Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo alisema leo kwamba mchezo huo utaanza Saa 2:00 usiku.
Wambura
amesema kwamba mechi nyingine zote za kufunga pazi la Ligi Kuu msimu 2017- 2018
zitachezwa kuanzia Saa 10: 00 jioni Jumatatu ya Mei 28, 2018 kwa timu zote 16
kuingia viwanjani kukamilisha raundi ya 30 na mechi 240 za msimu huu.
Wambura, amezitaja mechi hizo ni
kati ya Maji Maji ya Songea na mabingwa, Simba SC Uwanja wa Maji Maji mjini
Songea, Lipuli na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba na Tanzania Prisons dhidi ya
Singida United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Wakati Ligi
Kuu inamalizika Jumatatu, tayari Simba SC ndiyo mabingwa wakiwa wamejikusanyia
pointi 68 katika mechi 29, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 55 za mechi 29
na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC wapo nafasi ya tatu kwa pointi zao 51
za mechi 28 na leo wanacheza mechi yao ya 29 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa
Taifa.
Njombe Mji FC
tayari imeshuka Daraja kutokana na kuambulia pointi 22 katika mechi 29, wakati
Ndanda FC yenye pointi 26 za mechi 29 na Maji Maji FC yenye pointi 24 za mechi
29 pia mojawapo itashuka pia baada ya mechi za Jumatatu.
Wakati timu
mbili zitaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu Jumatatu, tayari African Lyon, KMC, JKT
Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance Schools ya Mwanza
na Biashara United ya Mara zimekwishapanda kuelekea ligi ya msimu ujao,
itakayokuwa na timu 20 ambayo ni ongezeko la timu nne.
No comments:
Post a Comment