Mohamed Salah wa Liverpool. |
KIEV, Ukraine
HATMA mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya yanafikia tamati kesho wakati Liverpool itakapoikabiri Real Madrid katika mchezo wa fainali utakaofanyika mjini hapa.
Ulikuwa
mchezo wa Kundi B kwenye Uwanja wa Bernabeu Novemba 4 mwaka 2014. Ni mfano
mkubwa wa mabadiliko ya jinsi mambo yalivyobadilika kwa Liverpool wakati mambo
yakiwa vile vile kwa Real Madrid.
Timu mwenyeji
itakuwa na wachezaji tisa katika kikosi cha kwanza huko Kiev leo Jumamosi,
wakati tofauti na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kwa upande wake.
Ni taarifa
kubwa kuhusu mchezo wa makundi, ambapo Liverpool ilipoteza kwa uchache kwa bao
la kipindi cha kwanza la Karim Benzema, lakini dakika 90 ziliihakikishia nafasi
Real Madrid.
Kipigo cha Liverpool
na kocha wa wakati huo, Brendan Rodgers aliyeweka kikosi dhaifu, kiichangia
kufungwa kwa timu hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 24
katika msimu uliopita.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid. |
Liverpool ilifungwa
bao 1-0 na kukawa na tetesi kuwa Rodgers aliisaliti historia na utamaduni wa
klabu hiyo ambayo imeshinda taji hilo mara tano na kuwaangusha maelfu wa
mashabiki wa timu hiyo.
Kwa upande wa
mabingwa watetezi Real Madrid, wenyewe walifika mapema kuendelea na mazoezi
hapa Kiev kwa ajili ya mchezo huo wa leo Jumamosi wakati mabingwa hao mara 12
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakitaka kutetea taji hilo kwa mara ya tatu
mfululizo.
Hatahivyo,
Real Madrid wasitarajie mteremko kwa Liverpool iko vizuri na ina safu kali ya
ushambuliaji, ambayo imetoa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika Ligi Kuu ya
England msimu uliomalizika.
Raphael
Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Luka Modric, Toni Kroos, Isco, Cristiano Ronaldo
na Benzema wataanza katika kikosi cha kwanza. Gareth Bale atakuwa katika benchi
lakini akitarajia kuingia wakati wowote.
Mchezaji bora
wa msimu, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane watakuwa katika safu ya
ushambuliaji wakati wakijaribu kuishtua Real Madrid wakirejea walivyofanya
mwaka 2014.
Salah,
Firmino na Mane wana magoli 29 kati yao msimu huu katika Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya na jumla wana mabao 90 wakati wakitengeneza utatu mtakatibu katika
ushambuliaji huku kocha wao Klopp akiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi leo
Jumamosi.
No comments:
Post a Comment