Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Viwango cha
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Vedastus Fabian (katikati waliokaa),
akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi na washiriki wa mafunzo ya usalama wa
vifurushi na mizigo inayosafirishwa kwa ndege, mara baada ya kufungwa kwa
mafunzo hayo jana katika Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo Jengo la Kwanza la
abiria la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. (Picha zote na Bestina Magutu wa TCAA).
Na
Bahati Mollel,TAA
WANAUSALAMA
wa viwanja mbalimbali vya ndege nchini, wameiva na kuimarika katika usalama wa
vifurushi na mizigo inayosafirishwa kwa njia ya ndege baada ya jana kufuzu
mafunzo yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Usafiri wa
Anga (ICAO), iliyofanyika kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo katika
Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBI).
Wakati
akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Viwango cha Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege Tanzania, Vedastus Fabian kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
amewataka wahitimu hao kutumia vyema ujuzi walioupata kwa kufanyakazi kwa
ufanisi na kuboresha kazi hiyo, ili kuepuka kupitisha mizigo hatarishi kwa
usalama wa usafiri wa anga.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Viwango cha
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Vedastus Fabian (aliyesimama)
akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya usalama wa vifurushi na mizigo (hawaonekani
pichani) wakati akifunga mafunzo hayo jana kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa TAA, kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo katika jengo la Kwanza la
abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).
“Tunavyojua mfumo wa usafiri wa anga duniani ni moja kwa hiyo tunavyoonesha usalama katika viwanja vyetu vya ndege hapa Tanzania kunajenga imani kubwa kwa mashirika ya ndege na wadau wote wanaofanya shughuli nakutumia viwanja vyetu vya ndege, hivyo tutaongeza wingi wa mizigo,” amesema Fabian.
Hata
hivyo, alitoa pongezi kwa wahitimu wote 19 kwa kuweza kufaulu vyema mafunzo
hayo, ambapo sasa watakuwa na weledi na ufanisi bora katika kazi hiyo.
Amesema
TAA inategemea mafunzo hayo yataleta manufaa na sio kuonesha vyeti ukutani kuwa
wamehitimu bali ni kuonesha ujuzi walioupata kutasaidia kutambua mizigo na
vifurushi vyenye matatizo ya kutishia usalama wa anga na kuongeza uhakika wa
safari za anga.
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya
Usafiri wa Anga (ICAO), Bw. Sunday Mweemba wa Zambia akielezea namna walivyotoa
mafunzo kwa wahitimu wa mafunzo ya usalama wa vifurushi na mizigo akishirikiana
na mkufunzi mwenzake Bw. Ernest Bongane wa Afrika ya Kusini, wakati wa kufunga
mafunzo hayo yaliyomalizika jana kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo
Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBI).
Hali
kadhalika amewataka washiriki kujiendeleza zaidi kwa kupata mafunzo mbalimbali ya masuala ya usalama katika
usafiri wa anga, kwa kuwa wahalifu wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali kila
wakati.
Naye
Kaimu Meneja wa Usalama wa TAA, Julius Misollow amesema washiriki wote
wameiva kwa kutambua na kubaini mizigo na vifurushi vyenye utata na vyenye
kutishia usalama wa usafiri wa anga nchini.
Missolow amesema wahitimu hao wataendelea na mafunzo ya ukufunzi, ambapo
wakihitimu wataisaidia mamlaka kwa kutengeneza wataalam zaidi wa masuala ya
usalama, ambao watapunguza gharama za kutumia wakufunzi kutoka nje ya nchi.
Naye
mmoja wa wakufunzi hao Sunday Mweemba kutoka Zambia amesema washiriki wote
wamepata mafunzo ya msingi kwa upana, ambapo yataisaidia nchi kufanya vizuri
katika usalama wa usafiri wa anga.
Washiriki wa mafunzo ya usalama wa
vifurushi na mizigo wakimsikiliza mgeni rasmi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Viwango cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Vedastus Fabian (hayupo
pichani) aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu, wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika
jana kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo katika Jengo la Kwanza la abiria
la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).
Mweemba amesema mafunzo haya yamekuwa yakitolewa nje ya nchi, lakini
ameishukuru menejimenti ya TAA kwa kujitoa kwa hali na mali na kufanikisha kuwaleta
wakufunzi hapa nchini ili wanausalama wengi zaidi waweze kushiriki, endapo yangeendeshwa
nje ya nchi wangeshiriki wawili au mmoja.
Kwa
upande wa wahitimu, Bw. Wenceslaus Sango ameishukuru menejimenti ya TAA kwa
kufanikisha mafunzo hayo, wakufunzi na mratibu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa
Anga nchini (TCAA), Bw. Burhan Majaliwa, ambapo wameahidi kuyatumia vyema kwa
faida ya taifa.
Washiriki
walioshiriki na viwanja wanavyotoka kwenye mabano ni pamoja na Mohamed Makau
(TAA Makao Makuu), Zalia Msangi na Stephen Magambo (Arusha); Philbert Lyimo,
Ahmed Zomboko, Thawabu Njeni, Rehema Mlanzi, Nuhu Kisweswe, Martha Kilunga,
Levina Valasa, Josephine Kahimba, Anna Myovela, Fatma Shomari na Stephen Ntambi
(JNIA);.
Wengine
ni Felister Lutonja (Shinyanga) Mathias
Gombo, Lilian Malero na Wenceslaus Sango (Mwanza) na Bebedict Ole Laput (Songwe).
No comments:
Post a Comment