Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Joseph Nyehende (aliyesimama) akifungua kozi
ya Usalama wa vifurushi na mizigo iliyoanza leo kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga
kilichopo Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA-TBI). (kulia) ni Bw. Sunday Mweemba wa Zambia na (kushoto)
ni Bw. Ernest Bongane wa Afrika Kusini, ambao ni wakufunzi. (Picha Zote na Bahati Mollel wa TAA).
Na Bahati Mollel, TAA
WANAUSALAMA
18 kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wametakiwa kuzingatia
mafunzo ya Usalama wa vifurushi na mizigo vinavyosafirishwa kwa ndege za mizigo, yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo kwenye jengo
la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI) Jijini Dar es Salaam.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Joseph Nyahende, ambapo amesema kuwa, mafunzo hayo yatasaidia zaidi kuongeza uelewa wa vifurushi na mizigo
hiyo inatakiwa kusafirishwa bila abiria kuambatana nao.
“Tunania
njema ya kuwatengeneza wanausalama wetu na hili darasa ni muhimu sana kwa ajili
yenu, hivyo tunahitaji mjifunze kwa faida yenu binafsi, taasisi na taifa kwa ujumla, kwani hamtaweza kuruhusu vitu visivyostahili kupita, kwani mtakuwa sasa mmepata
mafunzo ya kuvitambua,” alisema Bw. Nyahende.
Naye
mmoja wa wakufunzi Bw. Sunday Mweemba kutoka Zambia ameishukuru Menejimenti ya
TAA ya kuomba kozi hiyo kupitia taasisis ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO),
ambayo itawafanya wanausalama wake kutambua vitu vingi vinavyofanyika katika
viwanja vingine Duniani.
“Tumeona
ni jinsi gani menejimenti yenu ilivyojitoa kwa ajili yenu, na hii inatolewa na
ICAO na kupitia kazi yenu mnatakiwa kuwa makini zaidi na kuzijua sheria zote
zinazohusika na mizigo, na tunamatumaini hadi mwisho mtakuwa mmeweza kujijengea
uwezo,” alisema Bw. Mweemba.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa Usalama wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Julius
Misollow alisema mafunzo hayo ni ya kwanza, ambayo yanalengo la kuwajengea
uwezo wanausalama kukagua vifurushi na mizigo inayosafirishwa yenyewe bila
abiria kwa kutumia ndege za mizigo.
“Magaidi
wamekuwa wakitumia njia mbalimbali na wengine wanatumia mizigo au vifurushi
kufanya hujuma, hivyo tunaimani kwa mafunzo haya tutawajengea uwezo wa kutambua
mizigo, ambayo ni hatarishi, ingawa kwa Tanzania haijawahi kutokea tatizo hilo,”
alisema Bw. Misollow.
Hata
hivyo, amesema mafunzo hayo yatakuwa na mitihani na watakaofaulu kwa alama 70
wataendelea na kozi ya ukufunzi, ambayo itaanza baadaye kuanzia Mei 19, 2018.
Washiriki
wanaoshiriki na viwanja wanavyotoka ni pamoja na Philbert Lyimo, Ahmed Zomboko,
Thawabu Njeni, Rehema Mlanzi, Nuhu Kisweswe, Martha Kilunga, Levina Valasa,
Josephine Kahimba, Anna Myovela, Fatma Shomari na Stephen Ntambi (JNIA); Zalia
Msangi na Stephen Magambo (Arusha).
Wengine
ni Mathias Gombo, Lilian Malero na
Wenceslaus Sango (Mwanza); Bebedict Ole Laput (Songwe); na Felister Lutonja
(Shinyanga).
No comments:
Post a Comment