MADRID,
Hispania
ZINEDINE Zidane
anasema kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya “ni vinasaba vya Real
Madrid” baada ya kikosi chake kutinga kwa mara ya nne fainali ya mashindano
hayo katika kipindi cha miaka mitano.
Real ilipata
nafasi hiyo ya kucheza fainali ikisaka kushinda kwa mara ya tatu mfululizo taji
hilo baada ya Karim Benzema kufunga mara mbili na kuwawezesha mabingwa hao
watetezi kutoka sare ya 2-2 na kupata ushindi wa jumla wa 4-3 dhidi ya
Wajerumani Bayern Munich.
Real Madrid
tayari imeshuhudia wapinzani wao wakubwa Barcelona wakitwaa taji la La Liga
ndhini Hispania msimu huu, lakini Zidane anasema mashindano hayo makubwa Ulaya
mara nyingi timu yake inafanya vizuri, ambapo imeshatwaa taji hilo mara 12.
"Ni
vinasaba vya klabu yetu. Kamwe hatuachi kupambana hadi katika dakika ya mwisho,
kama walivyofanya Bayern usiku huu.”
Zidane alisema
Benzema alikuwa zaidi ya kuanza katika mchezo huo baada ya mshambuliaji huyo wa
Ufaransa alitolewa katika kipindi cha kwanza katika mchezo wa kwanza wa nusu
fainali uliofanyika Jinini Munich.
"alistahili
kufunga, alifanya kazi kwa bidii na kamwe huwa hana tabia ya kutojituma.
"Mchezo
wake mara zote huwa ni sawa na amekuwa mchezaji mwenye msaada mkubwa ketu.”
Baada ya
kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza nchini Ujerumani, Bayern Munich walikuwa
wakihitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano uliofanyika kwenye Uwanja wa Bernabeu
ili kutinga fainali lakini walijikuta wakimaliza mchezo huo kwa sare ya 2-2 na
kupata ushindi wa jumla wa mabao4-3.
Joshua
Kimmich aliifungia Bayern mapema kwa mkwaju wa umbali wa meta sita, kabla Karim
Benzema hajafunga kwa kichwa akiisawazishia Real Madrid akiunganisha wavuni
krosi ya Marcelo dakika nane baadae.
No comments:
Post a Comment