Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer. |
MUNICH,
Ujerumani
KIPA wa
Ujerumani Manuel Neuer yuko mbioni kuwa fiti kabla ya kuanza kwa fainali za
Kombe la Dunia baada ya kupona maumivu ya mguu yaliyomuweka kando kwa karibu
msimu mzima, alisema juzi kocha wa timu ya taifa Joachim Loew.
Akizungumza
wakati wa kuanza kwa mazoezi ya timu hiyo katika kambi yao kaskanzini ya
Italia, Loew alisema anauhakika kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye
ni nahodha wa timu ya Ujerumani, sehemu ya timu iliyotwaa Kombela Dunia 2014,
atacheza Urusi.
Neuer ambaye
ni kipa wa Bayern Munich hajacheza soka tangu alipovunjika mfupa wa mguu wake
Septemba mwaka jana, ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji na kumfanya kuwa
katika wasiwasi wa kucheza fainali hizo.
"alifanya
mazoezi wiki katika klabu ya Bayern, hapa anafanya mazoezi kamili na anaendelea
kuwa fiti, “alisema Loew alipozungumza na waandishi wa habari.
"Tutaangalia
mazoezi ya siku hadi siku. Ikiwa atakuwa fiti kwa asilimi 100 basi hakuna
ubishi atakwenda Urusi kwa ajili ya fainali hizo, na kama kutakuwa na tatizo
lolote, basi itabidi kuzungumza….”
Loew pia anatarajia
kurejea kwa Jerome Boateng katika kikosi chake wiki hii wakati beki huyo wa
kati akipona maumivu ya nyonga aliyoyapata mwezi uliopita.
"Kila
kitu kinakwenda vizuri kama kilivyopangwa na wiki ijayo tunamtarajia kushirii
katika mazoezi, “alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 58, ambaye mwezi huu
ameongeza mkataba wake utakaompeleka hadi mwaka 2022.
Wajerumani
wanajifua katika milima ya Alps nchini Italia kwa ajili ya maandalizi ya
kutetea taji la Kombe la Dunia, huku Loew akiwapongeza wachezaji wake wakati
wakiwa tayari kwa ajili ya kutetea taji lao.
"Hapa
kuna hali nzuri sana, uwanja mzuri, hoteli nzuri sana, sehemu ya kuchezea iko
katika hali nzuri sana, hivyo kila kitu kiko katika hali nzuri sana.”
Ujerumani
itaaendelea kubaki Italia hadi Juni 5, siku moja baada ya siku ya mwisho ya
kutangaza kikosi cha mwisho. Loew ina wachezaji 27 katika kambi hiyo huku wanne
wakitarajiwa kupigwa `panga’.
Ujerumani
itasafiri na kwenda kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki ugenini dhidi ya Austria
huko Klagenfurt Juni 2 kabla hajarejea na kukukabliliana na Italia kabla
haijarudi nyumbani kuikabili Saudi Arabia huko Leverkusen siku sita baadae,
wako katika Kundi F pamoja na Sweden, Korea Kusini na Mexico.
No comments:
Post a Comment