NEW YORK, Marekani
MARIA Sharapova (pichani) amerejea kwa kishindo katika mashindano
makubwa ya tenisi kwa kumtupa nje bingwa namba mbili kwa ubora duniani, Simona
Halep katika mashindano ya US Open.
Mrusi huyo alishinda kwa seti 6-4 4-6 6-3 mbele ya mashabiki
karibu 24,000 katika mchezo uliofanyika hapa.
Sharapova, 30, alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa
mashindano makubwa tangu alipokuwa akitumikia adhabu ya kifungo cha miaka 15 ya
kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Bingwa huyo wa mwaka 2006 alihitaji kufuzu ili kupangwa
katika ratiba kubwa ya mashindano hayo, ambapo sasa anashikilia nafasi ya 146
kwa ubora.
Sharapova alirejea katika mchezo huo Aprili lakini alikuwa
akipambana na maumivu ya nyama za paja, akicheza mara moja tu mwezi Mei, na pia
alikataliwa kucheza mashindano ya French Open.
Chama cha Tenisi cha Marekani kimechukua hatua tofauti, baada
ya kumpatia Mrusi huyo nafasi katika ratiba kubwa mjini New York, na alitumia
nafasi hiyo vizuri.
No comments:
Post a Comment