Na Mwandishi Wetu, Moshi
Josephat Joshua ndiye mshindi wa mbio za Kilifm
International Marathoni 2017 zilizofanyika jana mjini haa kwa uande wa wanaume
baada ya kutumia saa 1:04:18 huku Dickson Marwa akimaliza wa pili.
Marwa wiki iliyopita alimaliza wa kwanza katika mbio
za Bagamoyo Marathoni.
Kwa upande wa wanawake, Mkenya Shelmith Muruki
alimaliza wa kwanza kwa kutumia saa 1:16:13 huku mshindi wa Bagamoyo Marathon
kwa wanawake, Angel John alimaliza wa pili kwa kutumia saa 1:18;34 wakati Zakia
Mrisho alimaliza wa tatu kwa kutumia saa 1:19:82.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mbio hizo, Muruki
alisema kuwa zilikuwa nzuri na aliata ushindani mkali kutoka kwa Angel.
Joshua alishinda mbio hizo baada ya kuonesha jitihada
kubwa kwa kumpita mshindano wake aliyekuwa akiongoza kwa muda mrefu, Chacha
Musinde ambaye alionekana kama ndiye angeibuka na ushindi , lakini aliishia
kuwa watatu akipitwa hata na Marwa aliyekuwa katika nafasi la pili la uongozi.
Mshindi wa
kwanza katika mbio za kilometa 21 kwa wanawake na wanaume kila mmoja
aliondoka n ash 700,000 huku wa pili wakibeba 500,000 na watatu 300,000 wakati
wanne 200,000 na watano 100,000.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alikuwa
mgeni rasmi na alitoa zawadi na kukabidhi medali kwa washindi 10 wa uande wa
kike, ambao alitaka mbio hizo kuendeleza jitihada za kuendeleza viaji kwa
watoto wadogo ili kuiwaibua akina Filbert Bayi wapya.
No comments:
Post a Comment