Mkurugenzi wa Multchoice-Tanzania, Mahakarage Chande akionesha umari wa kupiga mpira kwamgongo wakati wa uzinduzi wa msimu wa Ligi Kuu za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.
|
Na Mwandishi Wetu
Wakati viguvugu la soka
ulimwenguni likizidi kupanda, Kampuni ya Multichoice Tanzania
kupitia king’amuzi cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka
ijulikanayo kama ‘Full Vyenga Bila Chenga’, ambapo watanzania kupitia DStv wataweza kushuhudia mubashara michuano
mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Ligi Kuu ya England (EPL) na ile ya Hispania ya La Liga pamoja na makombe mengine maarufu Duniani.
Pazia la Ligi Kuu ya England litafunguliwa Jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya
Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaoneshwa
mubashara kupitia DStv.
Akizungumza katika hafla
ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice
Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande amesema kuwa msimu huu
wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano
bora zaidi, huku wakiweza kufuatilia michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa
kwa lugha ya Kiswahili.
Waandishi wa Habari wakipiga bahati nasibu katika hafla hiyo. |
“Msimu huu watanzania,
kupitia DStv, siyo tu kwamba wataona michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni
mubashara, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu, yaani High Definition
na zaidi ya yote, tutawapatia fursa watanzania kufuatilia Ligi Kuu ya England kwa lugha ya Kiswahili”.
Amesema DStv imeendelea
kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vipindi na kurekebisha bei za vifurushi
ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kujionea matukio
mbalimbali muhimu katika Nyanja zote za maisha, ikiwemo michezo na burudani.
Ametoa mfano wa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga ambayo inaonekana yote katika
kifurushi cha Bomba. Pia baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya England (PL) pia
zitaonekana katika kifurushi cha Bomba.
Kwa upande wake, Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga bila
Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DStv, msimu huu wa soka wataweza kuliona soka
kwa muonekano bora zaidi, yaani bila chenga.
“Tunatambua kuwa washabiki wa soka
sasa wanataka walione soka vyema, kana kwamba nao wapo uwanjani. Kwa DStv, sasa
hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu anatoka jasho utaliona.
Hakuna wingu wala ukungu, ni ‘full vyenga bila chenga’ alisema Alpha.
No comments:
Post a Comment