Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Multchoice-Tanzania imewakabidhi zawadi zao
waandishi wa habari wawili walioshinda ving’amuzi vya DStv baada ya kucheza
bahati nasibu.
Waandishi hao, Abdallah Kaniki na Dennis Mpima walipata
zawadi hizo baada ya kuchezeshwa bahati nasibu kwa mara ya pili na kuwaibua
washindi hao wawili.
Awali, Multchoice-Tanzania waliendesha bahati nasibu, ambapo
waandishi wa habari 10 walijishindia jezi za timu mbalimbali za Ligi Kuu ya
England na zile za La Liga ya Hispania.
Droo hizo ziliendeshwa wakati wa hafla ya kuzindua vuguvugu
la soka ulimwenguni (Full Vyenga Bila Vyenga), ambalo linaanza mwikiendi hii
katika nchi tofauti.
Kwa mujibu wa mratibu wa hafla hiyo Shumbana James, Kampuni
ya Multchoice kupitia king’amuzi chake cha DStv imezindua kampeni maalum ya
Msimu Mpya ijulikanayo kama ‘Full Vyenga Bila Chenga’.
Mwanamke pekee aliyeshinda jezi akikabidhiwa jezi yake na msanii Rihama Ally. Kushoto ni Mkurugenzi wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande. |
Pazia la Ligi Kuu ya England litafunguliwa kesho Jumapili
Agosti 6 kwa mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao
utaoneshwa mubashara kupitia DStv.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka
iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema kuwa msimu huu wa soka, DStv
inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi.
No comments:
Post a Comment