Yafyeka Bei za Vifurushi Vyote! Wapenzi wa Kandanda ‘Meno Nje’
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusu bei mpya za vifurushi. |
Na Mwandishi Wetu
PANGA LA BEI LAFYEKA;
DStv Premium kwa 8.15%, DStv Compact Plus kwa 11.02%, DStv Compact kwa
16.11%, DStv Family kwa 9.09% and DStv Access (Bomba) kwa 4.88%
Katika kuhakikisha kuwa
wateja wake wote na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, Kampuni ya Multichoice Tanzania imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa
kufyeka bei za vifurushi vyake vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi
katika vifurushi vyake hususan vile vya bei ya chini!
Habari hiyo njema imetangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Multichoice Tanzania, Maharage Chande, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema bei hizo
mpya zitaanza kutumika rasmi Septemba mosi 2017.
“Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo ya uendeshaji wa
biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutusihi
tuangalie uwezekano wa kupunguza bei, tumechanganua kwa kina na tumeamua
kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha panga kwenye bei za vifurushi vyetu
vyote!” alisema Maharage.
Akifafanua kuhusu punguzo hilo, Maharage amesema kumekuwa na punguzo la hadi asilimia 16,
ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa ahueni kubwa watumiaji wa DStv.
Amezitaja bei mpya kuwa ni;
Bei Mpya za vifurushi vya DStv:
Kifurushi Bei ya
sasa Bei Mpya % Ya Punguzo
Premium TZS 184
000.00 TZS 169 000.00 8.15%
Compact Plus TZS 122
500.00 TZS 109 000.00 11.02%
Compact TZS 82
250.00 TZS 69 000.00 16.11%
Family TZS 42 900.00 TZS 39 000.00 9.09%
Access (Bomba) TZS
19.975.00 TZS 19 000.00 4.88%
Mara baada ya kutaja bei hizo Maharage aliwaambia waandishi
wa habari; “Kwa lugha ya mtaani wanasema ‘Vuma Vimekaza’ – ikimaanisha hali ya
kifedha imebana… Multichoice imelisikia hilo na kuamua kuwapa wateja wote wa
DSrv ahueni kubwa! Sasa kwa wateja wetu wa DStv, ‘Vyuma vimeachia’”
Maharage amesisitiza kuwa Multichoice itaendelea kuwasikiliza
wateja wake na kuhakikisha kuwa inatekeleza kile wanachohitaji wateja wake pale
inapowezekana.
“Wateja wetu walituomba tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye
king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel maalum kabisa ya Maisha Magic
Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania; wakatuomba tupunguze
bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana, na leo tena kwa mara
ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye vifurushi vya bei
ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta Laliga na Ligi kuu ya uingereza hadi kwenye
kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”.
“Kipekee kabisa Wananchi kupitia serikali wakatuomba tuongeze
nguvu kwenye kuinua vipaji vya vijana wetu wa kitanzania, tukasikia,
tukaitikia, tukaanza katika riadha ambapo tumemdhamini mwanariadha wetu
Alphonce Simbu. Sote tunajua matokeo yake, sasa Tanzania inahofiwa kwenye
ulingo wa riadha kimataifa! Haya yote tumefanya kwa sababu tunawasikiliza wateja
wetu, tunawasikiliza wadau wetu, tunawasikiliza Watanzania” alisema Maharage.
Wakati habari hii ikiwa ni njema kwa watanzania wote,
washabiki na wanazi wa kandanda wameonekana kufurahia Zaidi kwani kwa punguzo
hilo kuwa wataweza kushuhudia ligi kuu ya uingereza PL pamaja na ligi nyingine
kubwa ulimwenguni na makombe maarufu kama UEFA kwa bei nafuu zaidi.
Kwa maelezo Zaidi kuhusu bei mpya na vipindi mbalimbali
katika vifurushi vya DStv tembelea; www.dstv.com.
No comments:
Post a Comment