Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mghwira (pichani), atakuwa mgeni rasmi katika mbio za pili za kimataifa
za Kilifm Marathon zitakazofanyika Agosti 13, imeelezwa.
Mghwira hivi karibuni
aliteuliwa na Rais Dk John Magufuli kuwa mkuu wa mkoa huo akichukua nafasi ya
mtangulizi wake, Said Meck Sadick aliyeomba kujiuzulu.
Akizungumza kwa njia ya
simu kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro mratibu wa mbio hizo, Nelson Mrashani alisema kuwa mkuu huyo wa mkoa amethibitisha
kushiriki katika mbio hizo.
Alisema kuwa mbio hizo
mwaka huu zinatarajiwa kuwa za aina yake na kushirikisha wakimbiaji kibao
kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mbali na mbio za nusu
marathon ambazo ni za kilometa 21, pia kutakuwa na mbio za kilometa tano na
zile za watoto za kilometa 2.5 pamoja na zile za walemavu wa ngozi.
Mshindi wa kwanza wa mbio
hizo ataondoka na sh 700,000 wakati mshindi wa pili atabeba sh 500,000 huku
mshindi watatu atatwaa sh 300,000 na wanne sh 200,000.
Mrashani alisema kuwa
mwaka huu wanatarajia kushiriki zaidi ya wanariadha 1,000.
Mwaka 2015, alikuwa
mwanamke pekee aliyewania kiti cha Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance
for Change and Transparency (ACT), ambapo Magufuli wa CCM,
aliibuka mshindi wa kiti hicho.
No comments:
Post a Comment