NAIBU Mawaziri watatu wamesema kuwa kumalizika kwa Terminal Three ya
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kitatatua kero
zilizopo Terminal Two.
Kaimu Mkurugenzi JNIA, Johannes Munanka |
Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lamo
Makali wakati akitoa majumuhisho ya ziara yake na wenzake wawili, Hamad Masauni
na Edwin Ngonyani wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kwenye kiwanja hicho.
Manaibu hao walianza ziara hiyo kwa kutembelea maeneo mbalimbali katika
Terminal Two na kukutana na changamoto kibao, zikiwemo kero za msongamano wakati
wa hutoaji wa viza kwa abiria wanaowasili.
Kero nyingine ni abiria wanatakiwa kutoka nje ya kiwanja kubadili fedha
na kurudi ndani ili kupata huduma katika tawi la benki ya NMB lililopo ndani ya
kiwanja hicho ili kulipia viza.
Makani alisema itakapomalizika Termina 3 kero karibu zote zitamalizika
kwani jengo la kiwanja hicho linakidhi mahitaji yote muhimu, ambazo ni
changamoto katika jengo jingine.
Masauni alisema wizara yake itaongeza askari wa uhamiaji ili kuboresha
utendaji kazi kiwanjani hapo, kuongeza idadi ya mashine za viza na kubadilisha
mfumo wa utendaji ili kwenda na wakati.
Mhandisi Ngonyani alisema kuwa wanataka kuboresha miundo mbinu, ambapo
katika terminal 3 kutakuwa na uboreshaji wa maeneo mengi ili kuwahudumia
wasafiri wengi kwa mara moja.
Ngonyani aliishauri Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi kupunguza kutoa viza
abiria wanapowasili na badala yake zitolewe katika ofisi za balozi za Tanzania
nje ya nchi kama zifanyavyo nchi zingine
ili kupunguza msongamano.
Terminal Three. |
Terminal Two. |
Msafara wa Naibu Mawaziri walipotembelea JNIA |
No comments:
Post a Comment