Saturday, 5 August 2017

Mo Farah atetea ubingwa wa meta 10,000

LONDON, England
MO Farah kwa mara nyingine tena ametetea ubingwa wake wa dunia kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushinda mbio za meta 10,000 na kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia mjini hapa.

Akishangilia na umati wa watazamaji kama wakati ule alipofanya vitu vyake katika Olimpiki ilipofanyikia kwenye uwanja huo huo miaka mitano iliyopita, Muingereza huyo alionekana kama angeshindwa kabla ya kumaliza kwa nguvu na kushinda.

Hizo ndio mbio za mwisho za Farah za uwanjani za mashindano, tangu alipoanza kizzai cha dhahabu miaka saba iliyopita wakati alipofanya kweli kama sasa.

Tayari amedhihirisha kuwa bado yuko fiti na yuko tayari kushindana na wakali wengine, ambapo mtoto wake wa kiume na mabinti zake watatu waliungana naye uwanjani kushangilia wakati furaha zilipogubika eneo hilo.

Mganda Joshua Cheptegei aliambulia medali ya fedha wakati Mkenya Paul Tanui alimaliza katika nafasi ya tatu kwa kutumia dakika 26:49.51 ikiwa ni sekunde tatu nyuma ya muda binafsi bora wa Farah.

No comments:

Post a Comment