Na Mwandishi Wetu
TIMU za Yanga na Simba leo zinashuka kwenye Uwana wa Taifa kucheza
mchezo a Ngao ya Jamii ikiwa ni uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa Ligi Kuu
Tanzania Bara 2017/18 utakaoanza wikiendi ijayo.
Hii ni mechi ya tatu kwa kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina kukutana
na watani zake za jadi Simba, huku kocha huyo akifungwa mara mbili na watani
hao tangu alioanza kuifundisha Yanga.
Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Mzambia, George Lwandamina tangu achukue
nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm Desemba mwaka jana na mechi mbili
zilizopita zote alipoteza.
Januari 10, mwaka huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar – Yanga ilifungwa kwa penalti 4-2 na Simba baada ya sare ya 0-0 katika
mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Februari 26, mwaka huu, Simba ikatoka nyuma na kushinda 2-1 kwa mabao
ya Mrundi Laudit Mavugo dakika ya 66 na Shiza Kichuya dakika ya 81, baada ya
Simon Msuva kuanza kuifungia Yanga kwa penalti dakika ya tano.
Na mechi zote Lwandamina amefungwa na Simba ikiwa chini ya kocha
Mcameroon, Joseph Marius Omog akisaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja ambao wote
leo watakuwepo kwenye benchi la Simba,
Katika benchi la Yanga kuna mabadiliko kidogo, kocha msaidizi wa msimu
uliopita, Juma Mwambusi hayupo na nafasi yake imechukuliwa na beki na nahodha
wa zamani wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa.
Kwenye benchi la Simba, ameondoka kocha wa makipa Mkenya, Iddi Salim na
nafasi yake kuchukuliwa na golikipa wa zamani wa timu hiyo, Muharami Mohammed ‘Shilton’.
Kiungo Haruna Niyonzima leo ataibukia kwa mahasimu Simba, baada ya
miaka sita ya kucheza Yanga tangu alipojiunga nayo mwaka 2012 akitokea APR ya Rwanda.
Yanga pia haitakuwa mchezaji wake mahiri na aliyekuwa tegemeo katika safu ya
ushambuliaji, Simon Msuva aliyehamia Difaa Hassan El- Jadida ya Ligi Kuu ya
Morocco.
Mshambuliaji Ibrahim Hajib naye leo ataibukia kwa watani, Yanga baada
ya kuibukia timu ya vijana ya Simba na kupandishwa kikosi cha kwanza cha timu hiyo
alikopatia umaarufu. Simba pia haitakuwa na beki wake, Abdi Banda aliyehamia Baroka FC ya Ligi Kuu ya
Afrika Kusini.
Timu zote zilikuwa kambini upande wa pili wa Muungano wa Tanzania kwa
wiki nzima – Yanga walikuwa
kisiwani Pemba na Simba walikuwa Unguja na kabla ya mchezo wa leo, kila timu imecheza
mechi sita za kujipima na kila moja ilipoteza mchezo mmoja.
Simba ilifungwa 1-0 na Orlando Pirates, kabla ya kutoa sare ya 1-1 na
Bidvest Wits nchini Afrika Kusini, ikashinda 1-0 na Rayon Sport ya Rwanda, 1-0
na Mtibwa Sugar, 0-0 na Mlandege na kumalizia kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya
Gulioni FC, wakati Yanga ilishinda 5-0 na Moro Kids, 3-2 na Singida United,
ikafungwa 1-0 na Ruvu Shooting, ikashinda 2-0 na Mlandege, 1-0 na Chipukizi na
1-0 na Jamhuri.
Mara ya mwisho Yanga kuifunga Simba ilikuwa ni Februari 20, mwaka 2016
ushindi wa 2-0 uliotokana na mabao ya mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma
dakika ya 39 na Amissi Tambwe dakika ya 72, ambao kwa pamoja leo wanatarajiwa
kuiongoza tena timu hiyo.
REKODI YA SIMBA NA YANGA NJE YA LIGI KUU:
NANI MTANI JEMBE:
DESEMBA 13, 2014
Simba SC 2-0 Yanga
WAFUNGAJI:
SIMBA SC: Awadh Juma na Elias Maguri
NANI MTANI JEMBE:
DESEMBA 23, 2013
Simba SC 3-1 Yanga
WAFUNGAJI:
SIMBA SC: Amisi Tambwe dk 14 na 44penalti na Awadh Juma dk,
YANGA SC: Emmanuel Okwi dk87
KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:
JULAI 10, 2011
Yanga 1-0 Simba, Fainali
MFUNGAJI : Kenneth Asamoah dk 108
JANUARI 1975
Yanga Vs Simba; Fainali, 2-0
WAFUNGAJI: Gibson Sembuli na Sunday Manara
JANUARI 1992
Simba Vs Yanga; Fainali
1-1, Simba ilishinda kwa penalti 5-4
JULAI 27, 2008
Simba Vs Yanga; Mshindi wa Tatu
(Yanga haikutokea uwanjani, Simba ikapewa ushindi wa chee)
KOMBE LA HEDEX:
JUNI 30, 1996
Yanga Vs Simba 2-0
CCM Kirumba, Mwanza
WAFUNGAJI: Bakari Malima na Edibily Lunyamila
KOMBE LA HEDEX:
JULAI 13, 1996
Simba Vs Yanga 1-1, Taifa, Dsm
WAFUNGAJI:
SIMBA: Hussein Amaan Marsha kwa penalti
YANGA: Bakari Juma Malima
KOMBE LA TUSKER:
FEBRUARI 10, 2001
Yanga Vs Simba (fainali) 0-0
(Simba ilishinda kwa penalti 5-4, Uwanja wa Taifa)
MACHI 31, 2002.
Simba Vs Yanga 4-1
WAFUNGAJI:
SIMBA: Mark Sirengo dk. 3 na 76, Madaraka Selemani dk. 32 na Emanuel
Gabriel dk. 83.
YANGA: Sekilojo Chambua dk 16.
(Mechi hii ya fainali iliyohudhuriwa na rais mstaafu, Ali Hassan
Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo
kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa
makusudi, ili kuuweka sawa. Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na
kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu
aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na
mashabiki wa Yanga. Mwamuzi wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi
vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na
hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama
cha Soka Tanzania, FAT).
JULAI 2, 2005
CCM Kirumba, Mwanza. Fainali
Simba Vs Yanga, 2-0
WAFUNGAJI: Emmanuel Gabriel dk. 60, Mussa Hassan Mgosi dk. 72
AGOSTI 15, 2006
Simba Vs Yanga; Nusu Fainali, 1-1
WAFUNGAJI:
SIMBA: Emanuel Gabriel dk. 69
YANGA: Credo Mwaipopo 90
(Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 7-6)
DESEMBA 24, 2009
Yanga Vs Simba; Nusu Fainali, 2-1
WAFUNGAJI:
YANGA: Jerry Tegete dk 67, Shamte Ally dk 120
SIMBA: Hillary Echesa dk 78 (penalti)
(Uwanja wa mpya wa Taifa)
KOMBE LA MAPINDUZI:
Januari 10, 2017; Nusu Fainali
Simba 0-0 Yanga
Simba ilishinda kwa penalti 4-2
JANUARI 12, 2011
Simba Vs Yanga; Fainali 2-0
WAFUNGAJI: Mussa Mgosi dk 33, Shijja Mkinna dk 71
(Uwanja wa Amaan, Zanzibar)
KOMBE LA AICC:
JUNI 1989
Yanga Vs Simba SC 1-0
MFUNGAJI: Joseph Machella
APRILI 20, 2003,
CCM Kirumba, Mwanza
Yanga Vs Simba 3-0
WAFUNGAJI:
Kudra Omary dk. 30, Heri Morris dk 32 na Salum Athumani dk. 47
KOMBE LA CCM
JANUARI 19, 2003
Simba Vs Yanga 1-1, Dsm
WAFUNGAJI:
SIMBA: Jumanne Tondolo dk. 10
YANGA: Mwinyi Rajabu dk. 20
NGAO YA JAMII:
FEBRUARI 17, 2001
Yangs Vs Simba 2-1, Dsm
WAFUNGAJI:
YANGA: Edibilly Lunyamila dk. 47, AllyYussuf 'Tigana' dk 80.
SIMBA: Steven Mapunda 'Garrincha' dk.43
AGOSTI 18, 2010
Yanga vs Simba 0-0
(Yanga ilishinda kwa penalti 3-1)
WAFUNGAJI: Geoffrey Bonny, Stefano Mwasyika na Isaac Boakye kwa upande
wa Yanga na Mohamed Banka kwa Simba.
WALIOKOSA: Ernest Boakye kwa Yanga na Emanuel Okwi, Uhuru Suleiman na
Juma Nyosso kwa Simba.
AGOSTI 17, 2011
Simba vs Yanga 2-0, Dar
WAFUNGAJI:
Haruna Moshi ‘Boban’ dk 15 na Felix Sunzu dk 38.
KOMBE LA FAT
NOVEMBA 15, 2000
Yanga Vs Simba 2-1
Sheikh Amri Abeid, Arusha.
WAFUNGAJI:
YANGA: Aziz Hunter 40 na Vincent Tendwa
SIMBA: Ally Yussuf 'Tigana' dk.37
NOVEMBA 12, 2000
MARUDIANO KOMBE LA FAT
Simba Vs Yanga 1-0, Dsm
MFUNGAJI:
SIMBA: Ben Luoga dk.44
(Matokeo ya jumla yakawa 2-2 na Yanga ikatolewa kwa mikwaju ya penalti
5-4)
No comments:
Post a Comment