Wanariadha wakichuana katika moja ya mbio za marathon hivi karibuni. |
Na Mwandishi Wetu
KAMAPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imejitosa kudhamini mbio
za pili za kimataifa za Kilifm Marathon zitakazofanyika Agosti 13, imeelezwa.
Mratibu wa mbio hizo, ambazo zinaadaliwa na Kituo cha Michezo
cha Kilifm, Nelson Mrashani alisema jana kuwa SBL imethibitisha kudhamini mbio
hizo mwaka huu.
Alisema kuwa siku ya mkesha wa mbio hizo kutakuwa na sherehe
kubwa mjini Moshi, ambapo mbali na vinywaji pia kutakuwa na nyama choma na
muziki wa nguvu.
Kampuni zingine ambazo tayari zimeshatangaza kudhamini mbio
hizo za kila mwaka ni pamoja na Coca Cola, maji ya Kilimanjaro, Kilifm Radio na
zingine.
Mratibu wa mbio jizo, Nelson Mrashani |
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ametangaza
kuwa mgeni rasmi katika uanzisha wa mbio hizo, ambazo zitakuwa za umbel.i wa
kilometa 21, tano na zile za watoto za 2.5.
Mghwira hivi karibuni aliteuliwa na Rais Dk John Magufuli
kuwa mkuu wa mkoa huo akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Said Meck Sadick
aliyeomba kujiuzulu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira |
Alisema kuwa mbio hizo mwaka huu zinatarajiwa kuwa za aina
yake na kushirikisha wakimbiaji kibao kutoka ndani na nje ya nchi.
Mshindi wa kwanza wa mbio hizo ataondoka na sh 700,000 wakati
mshindi wa pili atabeba sh 500,000, huku mshindi watatu atatwaa sh 300,000 na
wanne sh 200,000.
No comments:
Post a Comment