Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA Miss Kinondoni Dayana Edward ndiye mlimbwende wa Tanzania
2016 baada ya kuwashinda wenzake 29 katika viwanja vya Rock City Mall juzi
usiku mkoani hapa.
Mashindano hayo makubwa kabisa hapa nchini yaliamuliwa na majaji
ambao ni Rita Mbelo,Catherine Kibaso,Sophia Masei,Raphael Siantini,Joe
Makanyaga,Eliza Kilili,Juma Sultan,Prashant Patel na Ramesh Shah.
Mashindano hayo yalianza kwa warembo kucheza nyimbo mbali mbali kabla
ya kutinga na mavazi ya ubunifu,ufukweni na vazi la jioni.
Jaji Shah aliweza kuwataja warembo walioingia 15 bora ambao ni
Anna Nitwa,Sia Pius,Lisa Ndolo,Grace Malikita,Eunice Robert,Regina
Ndimbo,Iluminata Dominic,Sporah Lulende na Maria Peter.
Wengine ni Maureen Ayoub,Queen Nazir,Julietha Kabete,Maureen
Kamanya na Abel John.
Patel aliwataja warembo walioingia 5 bora ambao ni Grace
Malikita,Anna Nitwa,Maria Peter,Julietha Kabete na Dayana Edward.
Jaji Prashant Patel aliweza kutangaza warembo walioingia tatu
bora, ambao ni Dayana Edward aliyeibuka mshidi, huku nafasi ya pili
ikachukuliwa na Grace Malikita wakati Maria Peter alimaliza watatu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo,Annastazia Wambura aliomba mshindi wa shindano hilo ajitahidi kuzingatia
nidhamu na uzalendo haswa pale atakapo wakilisha nchini katika mashindano ya
mrembo wa dunia.
Wambura alisistiza waandaji wa mashindano hayo waendelee kufuata
taratibu za mashindano na kuhakikisha wanatekeleza mikataba waliosaini na
warembo hao.
Wambura ameomba mashindano hayo yafanyike katika mikoa mengine pia
tofauti na hapa.
Dayana alikabidhiwa gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya sh
milioni 14.
No comments:
Post a Comment