Wachezaji na viongozi wa timu ya Mamelodi Sundowns wakishangilia na Kombe
la Ligi ya Mabingwa wa Afrika walilolitwaa licha ya kufungwa bao 1-0 na Zamalek
jana.
|
CAIRO,
Misri
MAMELODI
Sundowns imeweka historia mpya baada ya kutwaa kwa mara ya kwanza taji la Ligi
ya Mabingwa wa Afrika licha ya kufungwa bao 1-0 na Zamalek katika mchezo wa
marudiano wa fainali uliofanyika Alexandria.
Timu
hiyo ya Afrika Kusini ilitwaa taji hilo kwa kupata ushindi wa jumla ya mabao
3-1 baada ya kushinda 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye uwanja wao
kabla ya juzi kufungwa bao 1-0.
Hii
ni mara ya kwanza kwa timu ya Afrika Kuisni kutwaa taji la Afrika, ambayo kwa
mara ya mwisho ilitinga fainali mwaka 2001 wakati walipofungwa na wapinzani
wakubwa wa Zamalek, Al Ahly.
Zamalek
walipata bao hilo pekee katika dakika ya 62 lililofungwa na Stanley Ohawuchi
licha ya kutawala mchezo huo na kufanya mashabulizi kibao langoni mwa Sundowns.
Lakini
uzuiaji wa Sundows uliisaidia timu hiyo kuwabana wapinzani wao na kufaidika na
ushindi mnono wa mabao 3-0 walioupata katika mchezo wa kwanza na kuwawezesha
kutwaa ubingwa.
Zamalek
iliingia uwanjani katika mchezo huo ikiwa na matumaini kibao ya kubadili matokeo
hayo huku Bassem Morsi akiwasalimia wapenzi wa soka na kumshangilia kwa nguvu
wakati mchezo huo ukianza.
Lakini
walikuwa Sundowns ndio walikuwa wa kwanza kufanya shambulio la nguvu pake
mshambuliaji wake Mzimbabwe Khama Billiat alipopiga shuti lilipaa juu ya lango
la Zamalek katika dakika ya tano tangu kuanza kwa mchezo huo.
Zamalek
nusura wapate bao la kuongoza katika dakika ya 12 wakati Ohawuchi, ambaye ndiye
pekee aliyeongezwa katika kikosi hicho, alipenya kwa mabeki lakini alishindwa
kufunga baada ya kupaisha mpira.
Sundowns
ilipata pigo baada ya kipa wake namba moja Mganda Onyango alipolazimika kutoka
uwanjani baada akiwa katika machela baada ya kuumua kifundo cha mguu, na
kumuingia kipa wa akiba Wayne Sandilands katika dakika ya 28.
Lakini
hakuwa na kazi ngumu hadi dakika 15 zilipopita pale ilipombidi kuokoa mchomo
uliopigwa na nahodha wa Zamalek Ahmed Tawfik.
Zamalek
waliongeza presha katikati ya kipindi cha kwanza lakini walikutana na kizingiti
kikali kutoka kwa safu ya ulinzi kutoka kwa mabeki wa Sundowns na mara nyingi
walijikuta wakimwaka pale walipojaribu kufanya shambulio la kushtukiza.
Billiat,
Percy Tau na Anthony Laffor wote wangeweza kuifungia Sundowns baada ya kufanya
shambulizi ya kushtukiza, hasa katika dakika nane za nyongeza za kipindi cha
kwanza kufidia mpira kusimama ili kumpa matibabu Onyango.
Katika
kipindi cha pili, mchezaji wa Zamalek, Ramzy Khaled alipiga mpira wa adhabu
mara baada ya mapumziko kabla Ohawuchi hajapiga shuti nje ya eneo la penalti.
No comments:
Post a Comment