WAKATI wadau wa michezo Tanzania Bara wanasita kujitokeza kuchukua
fomu za kuwania uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Zanzibar
kumekucha baada ya kiongozi mmoja wa michezo kukata utepe kwa kuchukua fomu.
Kiongozi huyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAA), Abdulhakim
Cosmas kuchukua fomu leo akitaka ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TOC.
Rais wa TOC, Gulam Rashid amesema leo kuwa, Cosmas anawania ujumbe
wa Kamati ya Utendaji ya TOC.
Akizungumzia mchakato mzima wa kuchukua fomu ulioanza jana
Jumanne, Rashid alisema kuwa unaendelea taratibu na wadau wengi wa michezo
wanafika katika ofisi ndogo za TOC Zanzibar na kuchungulia na kuondoka.
“Watu bado wanasuasua kwani
baadhi yao wanakuja na kuondoka, “alisema Gulam
katika mahojiano maalum leo Jumatano.
Kwa upande wa Tanzania Bara, hadi leo jioni saa 10:00 wakati ofisi
za TOC zilizoko Mwanyamala jengo la Biashara Complex zikifungwa hakuna mdau
yeyote wa michezo aliyejitokeza kuchukua fomu yeyote.
Nafasi zinazowaniwa ni pamoja na Rais, Makamu wa Rais, Katibu
Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi, Mhazini Mkuu, Mhazini Msaidizi na wajumbe 10 wa
Kamati ya Utendaji.
No comments:
Post a Comment