Na Mwandishi
Wetu
WAPENZI wa
michezo na burudani za aina mbalimbali kupitia king’amuzi cha DStv kuanzia Novemba
mosi watafaidi uhondo huo kwa gharama nafuu, imeelezwa.
Meneja Uendeshaji wa Multchoice-Tanzania, Baraka Shelukindo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu punguzo la bei za vifurushi
vya king’amuzi chao.
|
Kwa mujibu wa
meneja muendeshaji wa Multchoice-Tanzania Baraka Shelukindo, hatua hiyo
imechukuliwa ili kuwapunguzia gharama wateja na kwa uhondo zaidi.
Shelukindo
alisema kuwa wameamua kunufaisha wateja wake kwa kufanya mapinduzi makubwa
kupitia punguzo la bei na kuongeza chaneli
8 kupitia huduma yake ya DStv.
Huduma hizo
mpya za punguzo la bei zitaanza rasmi kufanya kazi kuanzia tarehe Novemba mosi,
ambavyo ni DStv Premium, Compact Plus, Compact,
Family na Access.
DStv Premium imefanya
punguzo la asilimia 16, ambapo bei mpya sasa itakuwa sh 184,000 wakati bei ya
zamani ni sh 219,000 wakati DStv Compact Plus, imepunguzwa
kwa asilimia 17 na sasa itakuwa sh 122,500 (zamani 147,000) Compact ya
kawaida sasa ni sh 82,250
wakati zamani ni sh 84,500.
Meneja Mauzo wa Multchoice-Tanzania, Salum Salum akizungumza na waandishi wa habari huku Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Baraka Shelukindo akimsikiliza.
|
Alisema
sasa kifurushi cha familia, ambacho sasa kitakuwa sh 42,900 badala ya bei ya
awali ya sh 51,000 kwa mwezi.
Kifurushi cha DStv Bomba kitafaidisha wateja wake kwa ongezeko la
chaneli 3, na punguzo la asili mia 15, bei yake mpya ni sh 19,950. Punguzo hili
la bei kwa kifurushi hiki litaanza Novemba 15.
Alisema
kuwa wateja wataendelea kufaidi burudani ya hali ya juu ya vichekesho,
tamthilia, sinema, michezo na vinginevyo kutoka katika king’amuzi cha DStv.
Chaneli hizo
mpya zitakazorushwa ni Vuzu AMP, Lifetime, Discovery channel,Crime & Investigation, History channel na Africa Magic Showcase.
Waandishi wa habari wakiuliza maswali katika hafla hiyo ya kutangaza punguzo la bei za vifurushi vya DStv.
DStv Compact Plus, imeongezewa chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa
mpira wa miguu kupitia vipindi vya UEFA Champions Leagues, European
Football leagues na Europa league. Hizo
mechi zote zinapatikana kwenye stesheni za SuperSport
6 (SS6) na SuperSport 4 (SS4).
Kwa wapenzi wa filamu za kiafrika, watafaidi kupitia Nollywood , wapenzi
wa tamthilia zakilatino wataburudishwa
na telenovelas pamoja na filamu za Bollywood.
Bila kusahau sinema zitakazopatikana kupitia chaneli za ROK,
Eva Plus na B4U Movies.
No comments:
Post a Comment