LONDON, England
KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa timu
yake sasa inahitaji `kuangalia kwa kina hali iliyopo’ baada ya timu hiyo kutoka sare
dhidi ya Southampton ikishuhudiwa timu hiyo ikitoka sare mara ya tano mfululizo
bila ya kushinda.
Katika mchezo huo uliochezwa mapema leo Jumapili, Manchester City imerejea
kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya England licha ya kuondoka na sare dhidi
ya Southampton.
Wageni ndio walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo
lilipatikana baada ya pasi ya John Stones kumuwezesha Nathan Redmond kumzunuka Claudio
Bravo na kufunga bao lililojaa wavuni.
City waliimarika baada ya awali kuzomewa na mashabiki pale
walipopata bao la kusawazisha lililofunwa na mchezaji aliyeingia akitokea
benchi Kelechi Iheanacho kufuatia krosi fupi ya Leroy Sane.
Kikosi cha kocha Pep Guardiola kilitawala mchezo katika
kipindi cha pili lakini kipa wa Watakatifu Fraser Forster ndiye aliyekuwa
kikwazo kwa Man City kupata bao.
Man City inaoonoza kwa kuwa na pointi 20 sawa na Arsenal
iliyopo katika nafasi ya pili pamoja na Liverpool ya tatu huku City wakiwa juu
kutokana na tofauti ya uwiano wa mabao tu.
No comments:
Post a Comment