TIMU ya Chelsea leo imefanya kweli baada ya kuutumia
vizuri Uwanja wao wa nyumbani baada ya kuikandamiza Manchester United kwa mabao
4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Chelsea imemuumbua kocha wao waamani Jose Mourinho
ambaye kwa sasa anayeinoa Manchester United ambayo pia inashiriki katika
michuano ta lii ndoo ya Ulaya.
Katika mchezo huo unaoelekekea ukinoni kwenye Uwanja
wa Stamford Bridge, mabao ya wenyeji Chelsea yaliwekwa kimiani na Pedro katika dakika ya kwanza wakati bao la
pili liliwekwa nyavuni na Cahill katika dakika ya 21 huku Hazard akicheka na nyavu katika dakika ya 70 Kante
akifuna katika dakika ya 70 na na 75.
Katika mchezo uliotanulia, Manchester City imerejea kileleni
katika msimamo wa Ligi Kuu ya England licha ya kuepata sare ya tano dhidi ya Southampton
na kuondoka na pointi moja.
Wageni ndio walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilipatikana
baada ya pasi ya John Stones kumuwezesha Nathan Redmond kumzunuka Claudio Bravo
na kufunga bao lililojaa wavuni.
City waliimarika baada ya awali kuzomewa na mashabiki pale
walipopata bao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji aliyeingia akitokea
benchi Kelechi Iheanacho kufuatia krosi fupi ya Leroy Sane.
Kikosi cha kocha Pep Guardiola kilitawala mchezo katika
kipindi cha pili lakini kipa wa Watakatifu Fraser Forster ndiye aliyekuwa
kikwazo kwa Man City kufunga.
No comments:
Post a Comment