Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu wa TOC,
Filbert Bayi wakiwa na Kifimbo cha Malkia wakati kilipotua Ikulu jijini Dar es
Salaam mwaka juzi.
|
Na Mwandishi Wetu
KIFIMBO cha Malkia wa
Uingereza kinatarajia kuwasili nchini Aprili 8 mwakani ikiwa ni maandalizi ya
Michezo ya 21 ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Gold Coast, Australia 2018
kuanzia Aprili 4 hadi 15.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazopitiwa
na mbio hizo za kifimbo cha Malkia, ambacho hupokewa na mkuu wa nchi.
Bayi alisema kuwa maandalizi
ya kupokea kifimbo hicho yataanza mwezi ujao wakati TOC itakapokutana na wadau mbalimbali
ili kuteua kamati maalum ya itakayoratibu ujio wa kifimbo hicho.
Aliwataja baadhi ya wadau
hao kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
Kamanda wa Polisi wa mkoa, ofisi ya Mambo ya Nje na wengine wengi.
Alisema kuwa wanasaka
wadhamini ili kufanikisha ujio wa kifimbo hicho, ambapo zinahitajika zaidi ya
sh milioni 60 wakati wenyeji Australia wameipatia TOC kiasi cha dola z Marekani
3,000 tu, ambazo ni sawa na sh. Milioni 6.
Bayi alisema kuwa wadhamini
hao wanatarajia kuwa ubalozi wa Uingereza, Kampuni ya vinywaji ya Peps Cola
ambayo mara ya mwisho kilipokuja kifimbo hicho walisaidia sana, Acacia na ITV,
Azam TV na vyombo vingine vya habari.
Alisema kuwa wadhamini
wakubwa ni pamoja na British Council, Ubalozi wa Uingereza, Peps na Shirika la
Kimataifa la Watoto Duniani, Unicef.
Mwaka 2014 Kifimbo cha
Malkia kilitua nchini na kukimbizwa katika barabara mbalimbali za jijini Dar es
Salaam kabla ya kutua Ikulu, ambako kilipokewa na Rais wa Awamu ya Nne Jakaya
Mrisho Kikwete na baadae kuzungumza na wana michezo.
Kifimbo hicho kilikuwa
maalum kwa ajili ya Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Glasgow, Scoland
Michezo hiyo itafanyikia
katika jiji la Gold Coast City, lililopo kusini ya Jimbo la Australia la
Queensland, ambapo hii itakuwa ni mara ya tano kwa Australia kuandaa, ambapo
pia iliwahi kuandaa mwaka 1938 Sydney, 1962 Perth, 1982 Brisbane na mwaka 2006
Melbourne.
No comments:
Post a Comment