NDOLA, Zambia
NIGERIA imeanza kwa ushindi
kampenzi zake za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 Kanda ya Afrika baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Zambia katika mchezo wa Kundi
B uliofanyika hapa.
Kwa ushindi huo, Nigeria
wanaoongoza katika kundi lao, baada ya vigogo wengine wa Afrika Algeria kubanwa
na kulazimishwa sare na Cameroonin na kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Kwingine, Misri iliifunga
Congo 2-1 katika mchezo wa Kundi E uliofanyika Brazzaville huku katika Kundi A,
Tunisia ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea.
Katika mchezo wa Nigeria,
mabao yao yalipatikana katika kipindi cha kwanza yaliyofungwa na nyota wanaong’ara katika timu
zinazoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
Mshmabuliaji wa Arsenal Alex
Iwobi ndiye aliyeiweka mbele Super Eagles baada ya kufunga bao katika dakika ya
32.
Mshambuliaji wa Manchester
City Kelechi Iheanacho aliongeza uongozi huo wa City dakika 10 baadae na
kukiweka kikosi cha kocha Gernot Rohr kuwa mbele kwa mabao 2-0.
Nigeria nusura ipate bao la
tatu na ingeweza kuwa mbele kwa mabao 3-0 katika mchezo huo uliofanyika Ndola
kama sio nahodha wake John Mikel Obi kukosa bao katika kipindi cha pili, baada
ya kupiga shuti la mbali lililookolewa kifundi na kipa wa Zambia Kennedy
Mweene.
Zambia ilipambana kiume na
juhusi zake zilileta mafanikio pale ilipopata bao la kufutia machozi katika
dakika ya 71 kupitia kwa Collins Mbesuma.
Pamoja na presha kutoka kwa timu
mwenyeji, Nigeria iligangamala na kuendeleza rekodi ya ushindi ugenini na
kuongoza katika Kundi B, likiwa ni moja ya makundi magumu katika mechi hizo za
kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Timu nyingine mbili katika
Kundi B, Algeria, ilimchezesha mchezaji wake anayekipiga Leicester City, Riyad
Mahrez na Islam Slimani, wakati ikicheza na Cameroon na kutoka sare ya bao 1-1.
Muargeria El Arabi Soudani aliiweka
mbele timu yake katika mchezo uliofanyika Blida, lakini yule wa Cameroon, Benjamin
Moukandjo ilisawazishwa kabla ya mapumziko.
Pia katika mchezo mwingine
uliofanyika Jumapili, Misri ilikwenda kileleni katika Kundi E kwa ushindi wa
mabao 2-1 ugenini dhidi ya Congo Brazzaville, wakifuatiwa na suluhu ya Ghana
nyumbani dhidiya Uganda katika mchezo uliofanyika Ijumaa.
Wenyeji waliuanza mchezo huo
kwa nguvu wakati mchezaji wake anayecheza soka la kulipwa Ufaransa Ferebory
Dore alipofunga bao la kuongoza kwa Congo Brazzaville katika dakika ya 24.
Hatahivyo, kikosi kabambe
cha Misri kilijibu mapigo kwa mshambuliaji wake anayecheza soka la kulipwa Roma
Mohamed Salah kusawazisha dakika nne kabla ya mapumziko na matokeo kuwa 1-1.
Katika dakika ya 58, Salah alibadili
matokeo wakati alipomtengenezea mcherzaji wa Al Ahly, Abdallah El-Said aliyefunga
na kufanya matokeo kuwa 2-1 kwa Misri.
Tunisia iliibuka na ushindi
wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea katika mchezo wa Kundi A huko Monastir uliofanyika
baadae Jumapili.
Mabao ya kipindi cha pili
kutoka kwa Aymen Abdennour na Ahmed Akaichi yaliipatia timu hiyo ya Afrika
Kaskazini ushindi ulioiweka katika nafasi ya pili katika Kundi A, nyuma ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyoifunga Libya 4-0 Jumamosi.
Washindi watano wa makundi
ndio watakaofuzu kwa ajili ya kuliwakilisha bara la Afrika katika fainali za
Kombe la Dunia zitakazofanyika Urusi mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment